Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KUNDUCHI WAANDAMANA KWENDA POLISI

Picha za waandamanaji wakielekea kituo cha polisi.
KAMERA ya GPL imewashuhudia wakazi wa Kunduchi jijini Dar es Salaam, wakiandamana kuelekea vituo vya Polisi vya Wazo na Mtongani, baada ya kudai kuwa ndugu zao wamekamatwa wakiwa hawana makosa na kupelekwa kituoni.
Wakizungumza na GPL baadhi ya waandamanaji walisema difenda tano za Polisi zilikwenda eneo hilo na kuanza kukamata watu ovyo kwa madai kuwa ni wahuni na wavuta bangi.
Dereva mmoja wa bodaboda alisema kawaida ya Polisi hao hufika na kuwakamata wahuni, wavuta bangi na vijana walio katika makundi ya uhalifu, ila kilichotokea ni wahuni hao kushtuka na kukimbia, ndipo polisi wakaaanza kukamata watu hovyo hata wasiohusika.

 (Habari/Picha na: Gabriel Ng’osha/GPL)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright 2025 EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG | Designed By Code Nirvana
Back To Top