Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Mkoma, akizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu akihutubia katika uzinduzi huo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick
Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi Mwalimu Lucy Mshomi wa Shule ya
Wasichana ya Kifungiro kutokana na mchango mkubwa kwa wanafunzi wao.
Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta, Deus Mndeme.
WANAFUNZI
wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St Mary's ya Mazinde Juu iliyopo
mkoani Tanga wameibuka vinara wa shindano la uandishi wa barua
lililoshirikisha wanafunzi wa shule mbalimbali nchini katika kuadhimisha
siku ya posta duniani.
Shindano hilo la uandishi wa barua limeratibiwa na Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na umoja wa posta duniani.
Akizungumza Dar es saalam leo katika hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya posta duniani, Mkurugenzi Mkuu wa Posta nchini, Deus Mdeme alitoa pongezi kwa washindi hao na walimu wao kwa kufanikiwa kuibuka videdea ambapo mshindi wa kwanza ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya barua ya kimataifa yatakayofanyika baadaye mwaka huu nchini Uswisi.
"Madhumuni ya shindano hili ni kuwajengea uwezo vijana ambao hawajazidi miaka 15'' alisema Mdeme.
Katika Shindano hilo la uandishi wa barua jumla ya washindi kumi walipatikana, huku St Mary Mazinde juu wakiibuka videdea kwa kutoa washindi wawili huku mshindi wa pili akitoka Shule ya Sekondari ya Lufingilo mkoani humo ambapo walikabidhiwa vyeti na zawadi mbalimbali.
Aidha katika kuadhimisha siku hiyo ya posta duniani, yenye kauli mbiu isemayo posta inachukua nafasi yake katika mageuzi ya sekta ya mawasiliano imeadhimishwa kwa kuelezea malengo na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Posta Tanzania.
Wakati huo huo Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Patrick Makungu kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa, alielezea mafanikio na changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekta ya Posta Tanzania katika kufanikisha malengo yake.
Vilevile alitumia nafasi hiyo kuhamasisha wanafunzi wengi zaidi kushiriki katika shindano hilo linaloandaliwa na umoja wa posta duniani na kuwataka wadau wa posta nchini kushirikiana na shirika hilo ili likue na kutoa huduma kwa jamii baada ya kubadilisha ufumo wa utoaji huduza zake kwa kutumia zaida Tehama.
Post a Comment