Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Tano la Kimataifa la
kujadili matumizi ya Nishati itokanayo na joto ardhi katika Nchi za
Afrika zinazopitiwa na bonde la ufa. Kongamano hilo limeanza leo Oktoba
29, 2014 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, akizungumza kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt Bilal, kufungua kongamano
hilo.
Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya waliohudhuria kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
Baadhi
ya washiriki wa Kongamano hilo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika
waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo
baada ya ufunguzi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya washiriki wakati akiondoka eneo hilo baada ya
kufungua kongamano hilo.
Makamu
wa Rais Dkt. Bilal, akifurahia burudani ya ngoma ya asili ya kabila la
wamasai wakati akiondoka katika Ukumbi wa AICC baada ya kufungua rasmi
Kongamano hilo. Picha na OMR
Post a Comment