 |
Wachezaji wa timu ya Mwadui FC,
wakishangilia goli lililofungwa na Bakari Kigodeko, katika mchezo wa
ligi
daraja la kwanza dhidi ya Panone FC, uliofanyika kwenye Dimba la
Ushirika, mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. mchezo huo ulimalizika kwa
sare ya 1-1. |
 |
Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kwenye
dimba la Ushirika, wakifuatilia mchezo kati ya Mwadui na
Panone. |
 |
Mashabiki wa Panone wakishangilia goli la
kusawazisha lililopatikana katika dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza,
likifungwa na Tony Kigundu. |
 |
Shangwe
zikaendelea |
 |
Kocha msaidizi wa Klabu ya Mwadui, Amri
Said, akizuiwa na mwamuzi wa mezani, Thomas Mkombozi wakati akijaribu
kutaka kumfuata mshika kibendera namba moja akipinga maamuzi akipinga
maamuzi ya kuingia kwa bao la Panone FC alilodai lilikuwa la
utata. |
 |
Ubabe
ukatumika... |
 |
Hapa akimrudisha Kocha wa Mwadui FC,
Jamhuri Kiwelo 'Julio' katika eneo lake. |
 |
Benchi la Ufundi la Mwadui FC, wa kwanza
kushoto ni kocha mkuu Jamhuri Kiwelo 'Julio', kulia.
|
 |
Julio akitoa maelekezo kwa mchezaji
wake |
 |
Mwokota mipira akiwa katika
pozi. |
 |
Sehemu ya Jukwaa kuu likiwa limesheheni
mashabiki |
 |
Wachezaji wakitoka
mapumziko |
 |
Mmoja wa viongozi wa Benchi la Ufundi la
Mwadui FC, aliamua kuwavaa maaskari wa Jeshi la
Polisi. |
 |
Kocha Jamhuri Kiwelo katikati ya dimba |
 |
Waamuzi wakiondolewa uwanjani kwa Ulinzi
mkali muda wa Mapumziko. |
 |
Kocha wa Panone FC, Maka Marwisi, akitoa
maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa
mapumziko. |
 |
Hivi karibuni Bodi ya Ligi iliamuru
kujengwa Uzio kuzunguka eneo la ndani ya Uwanja 'Pitch" kwa ajili ya
usalama wa wachezaji lakini cha kushngaza kama inavyoonekana hapo,
hizo ni pikipiki "Bodaboda" zikiwa zimeegeshwa ndani ya uzio huo,
jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa wachezaji
hao. |
 |
Jamhuri Kiwelo akitoa maelekezo kwa
wachezaji wake. |
 |
Heka heka za kuwania mpira ukiendelea
katika mchezo huo mkali. |
 |
Mchezaji wa Panone FC, akikimbilia mpira
|
 |
Wachezaji wa Panone FC, wakitoa huduma
kwa mchezaji wao aliyeumia. |
 |
Hapa wakiwa wamembeba....hili ni tukio la
kushangaza na la aibu kweli.. |
 |
Benchi la ufundi la Panone FC,
walipochukua jukumu ya timu ya usalama ya msalaba
mwekundu. |
 |
Panone FC, wakifanya
mabadiliko |
|
|
Mwadui FC wakifanya mabadiliko.
Na Dixon
Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya
kaskazini. |
on Friday, October 17, 2014
Post a Comment