Mwanamke mmoja Kilimanjaro amekamatwa na polisi akidaiwa kumkata mtoto wake mwenye umri wa miaka nane nyama ya paja na kuichoma mithili ya mshikaki.
Mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Dafrosa Massawe anadaiwa kufanya unyama huo mwishoni mwa wiki na majirani wanasema mama huyo alifanya hivyo akiwa amelewa.
Kamanda wa Polisi Kilimanjaro Koka Moita alisema mwanamke huyo ataendelea kushikiliwa hadi uchunguzi wa tuhuma hizo utakapokamilika kabla ya kupelekwa mahakamani.
Akizungumza na Gazeti la MWANANCHI katika hospitali ya Kibosho mtoto huyo alisema hafahamu kosa alilofanya hadi mama yake ambaye ni mtengenezaji wa pombe za kienyeji kumfanyia kitendo hicho.
Alisema mama yake alirudi nyumbani usiku na kumkuta amekaa na kumsalimia kisha akamwomba chakula wakati akijua hakuna na baadae aliingia jikoni na kuchukua kisu kisha kumkata nyama kwenye paja lake baada ya kumwambia alishinda na njaa siku nzima.
Alisema baada ya kuikata aliichoma kama mshikaki na ilipoanza kufuka moshi na kutoa harufu aliitoa jikoni na kumwekea mtoto huyo puani ili avute harufu yake.
Post a Comment