Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zubeir Mtemvu.
Baada ya watu kuja na Ushahidi mbalimbali juu ya umri wake Sitti Mtemvu kupitiapage yake ya facebook ameandika.
Habari
tulizozipata hivi punde kutoka kwenye ukurasa wa facebook wa Miss Tz
2014 Sitti Abbas Mtemvu ameandika Kujivua Taji hilo la Miss Tz 2014
kutokana na anachokiita yeye kusakamwa, kusemwa na wadau mbalimbali wa
urembo na Watanzania kwa ujumla kutokana na Kudanganya Umri kitu ambacho
ni kinyume na taratibu za mashindano hayo ya urembo Nchini..
Tunaendelea
Kufuatilia habari hii kwa kina kuweza kufahamu kama ni kweli amejivua
taji hilo maana ukishangatwa na Nyoka hata Jani likikugusa unashtuka
sasa inawezekena kaamua kuandika hivyo ili kuudanganya tena Umma wa
watanzania ili apate likizo ya kutokuchunguzwa na BASATA mara baada ya
Idara hiyo kupewa maelekezo ya Kumchunguza na kupumzika kwa Maneno ya
Watanzania ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kupaza sauti ambayo
kiukweli Imeonyesha kuwa Miss Tz 2014 alidanganya Umri wake.
credit: Lukaza blog
Post a Comment