Katika hali isiyokuwa ya kawaida,
mpigadebe maarufu katika kituo cha mabasi cha mbalizi wilayani mbeya
amenunua mbuzi wawili na bidhaa nyingine za aina mbalimbali zenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja na kuzipeleka kwenye vituo vya
watoto yatima kama zawadi huku akiwaasa watoto hao kutoshawishika
kwenda kupiga debe kwenye vituo vya mabasi.
Mpigadebe maarufu katika kituo cha mabasi cha mbalizi, Anganile
Mwamuluma Andrea ambaye amefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 20
ameushangaza umma wa wakazi wa mbeya baada ya kuamua kununua mbuzi
wawili, mchele, maharagwe, sabuni, mafuta ya kupikia na mahindi na
kupeleka bidhaa hizo katika vituo viwili vya watoto yatima ambako
amezitoa kama zawadi kwa watoto hao, huku akiwaasa kutoshawishika
kujihusisha na kazi ya kupiga Debe kwenye vituo vya mabasi.

Walimu wa watoto hao wameeleza kushtushwa na kitendo cha mpigadebe
huyo, lakini wakasema kuwa ni mfano Bora wa kuigwa kwa vijana
wanaofanikiwa kukumbuka mazingira walikotoka, huku wakiwahimiza wazazi
kuongeza upendo kwa watoto wao ili kupunguza wimbi la watoto wanaoishi
katika mazingira magumu nchini.
Baadhi ya watoto ambao wamepokea msaada huo, wamemshukuru mpigadebe
huyo na kuwataka watu wengine kupata funzo la kuthamini na kuwapenda
watoto ikiwa ni pamoja na kuwaandalia mazingira mazuri ya kujitegemea.
ITV
Post a Comment