HALI bado
tete! Polisi wa Kituo cha Magomeni jijini Dar, wamemkamata baba mmoja
aliyetambuliwa kwa jina moja la Omar baada ya kupokea kipigo ‘hevi’
kutoka kwa raia wenye hasira kali akihusishwa na utekaji wa denti wa
Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere iliyopo maeneo hayo.
Denti
wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere, Magomeni (mwenye sare za shule)
aliyenusurika kutekwa na njemba inayotambuliwa kwa jina moja la Omar.
Tukio
hilo lililokusanya kadamnasi lilijiri wikiendi iliyopita,
Magomeni-Kagera, Dar wakati mwanafunzi huyo akitokea shuleni.Kwa mujibu
wa mashuhuda, denti huyo alipofika eneo hilo, baba huyo alimsalimia na
baada ya kujibiwa salamu yake alianza kumchombeza kwa maneno
matamu-tamu.
Baadhi ya raia wenye hasira kali waliotoa kipigo ‘hevi’ kwa Bw. Omar wakiwa wametanda eneo la tukio. Akizungumza
na Uwazi lililofika eneo la tukio ndani ya ‘dakika sifuri’, denti huyo
aitwaye Laila alisema licha ya kuitikia salamu ya jibaba huyo na
kumuamkia bado aliendelea kumchombeza na kila alipojaribu kumkwepa
ilishindikana.Makamanda wa Polisi waliofika eneo la tukio kumuokoa mtuhumiwa.
Njemba
huyo alivuka mipaka na kumshika mkono na kutaka kumvutia ndani ya gari
lililokuwa karibu yake ndipo Laila alipoamua kupiga mayowe ya kuomba
msaada na hatimaye kuokolewa na wasamaria wema waliokuwa wakipita njia.”
Mtuhumiwa (Omar) akiwa ndani ya gari mara baada ya kipigo.
Mwanafunzi
huyo aliendelea kusema: “Alianza kunifuatilia tangu kule, akanisalimia
hujambo nikamjibu sijambo, akaniambia tena kwenu hawajambo, nikamjibu
hawajambo, akaendelea kuniambia eti, nimfuate akanipe lambalamba, mimi
nikakataa kwa sababu mama alinikataza kukubali kupewa lifti na vitu
vingine kutoka kwa watu nisiowajua tangu aliposikia habari za watoto
kutekwa na Noah nyeusi.Wasamaria wema wakimuokoa mtoto huyo.
“Kila
kitu nilimkatalia lakini yeye akawa anaendelea kuniambia maneno yake na
kuanza kunivuta ndipo nikaona sasa naenda kufa hivyo ikanibidi nipige
kelele ndiyo watu wakatokea na kumkamata kisha kuanza kumpiga mpaka
walipofika polisi.”
Gazeti
hili lilizungumza na mtuhumiwa aliyekuwa amehifadhiwa ndani ya gari,
alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo alimuomba paparazi wetu kabla ya
yote kwanza amuokoe na kifo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali.Binti akiwa kwenye gari mara baada ya kuokolewa.
“Chondechonde
ndugu yangu, naomba kwanza mnilindie usalama wangu, hao jamaa wanataka
kuniua bila sababu, mimi wala sikuwa na nia mbaya na huyo binti
wananizushia tu, nilikuwa namsalimia tu,” alisema Omar kupitia upenyo
mdogo wa juu ya dirisha la gari alilohifadhiwa.CHANZO GPL
Post a Comment