Profesa Athuman Juma Livigha enzi za uhai wake.
MAUAJI ya
aliyewahi kuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Athuman
Juma Livigha (63) yaliyotokea nyumbani kwake, Bunju ‘B’, Septemba 30,
mwaka huu kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana yameibua mengine
ambapo sasa baadhi ya ndugu wamemtaja mwanamke mmoja kuwa huenda
anahusika.Wakizungumza na Uwazi siku ya mazishi ya profesa huyo wiki
iliyopita, ndugu hao bila kutaka jina la mwanamke huyo walisema kwa
asilimia kubwa mwanamke huyo aliyekuwa haelewani na marehemu anatakiwa
kufuatiliwa vizuri nyendo zake.
“Huyo
mwanamke alikuwa karibu sana na marehemu lakini ghafla akapotea, akawa
haonekani na tukasikia yupo tu hapa Dar. Kinachotushangaza hata katika
msiba wa profesa hajafika.
“Ni kwa nini kipindi hiki awe muoga wa kuja wakati anafahamika na
sisi wanafamilia tunamjua?” alihoji mmoja wa wana ndugu hao ambaye
hakuwa tayari kutaja jina lake.
Mwili wa Profesa Athuman Juma Livigha ukiswaliwa kwa ajili ya
mazishi. Kwa mujibu wa majirani wa marehemu, siku ya tukio walisikia
mlio wa risasi mara moja na sauti ya marehemu ikisema uwiii baadaye
kukawa kimya, ndipo kesho yake mwili wake ukaonwa na mfanyakazi wake
anayetunza bustani ambaye anaishi jirani na nyumbani kwa marehemu.
Uchunguzi wa Uwazi ulionesha kuwa, siku ya tukio marehemu alifika
nyumbani kwake saa tatu usiku na kuegesha gari ndani kisha aliingia
ndani na kuwasha taa za ndani na nje.Baadaye marehemu alitoka nje kwa
lengo la kuchukua mizigo ndani ya gari, ndipo wakati anaingia watu
wasiojulikana walimpiga risasi akiwa mlangoni.
Mwili wa Profesa Athuman Juma Livigha ukipelekwa makaburini kwa ajili
ya mazishi. Ilibainika kuwa baada ya kupigwa risasi, alijitahidi
kukimbia ili kujiokoa lakini aliishiwa nguvu akadondoka chini na wauaji
walimchukua na kumlaza barabarani karibu na kwake kisha kumfunika kwa
kanga.
Marehemu Profesa Livigha alizikwa Alhamisi iliyopita kwenye Makaburi ya Bunju ‘B’ jijini Dar es Salaam.
Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.
CHANZO GPL
Post a Comment