Mwili wa msanii 'YP' ambaye alifariki usiku wa kuamkia juzi katika hospitali ya Temeke Jijini Dar es salaam, umezikwa jana kwenye makaburi ya Chang'ombe.
Mwili wa marehemu YP uliagwa jana mchana huko TCC Sigara Chang'ombe ambapo wasanii na wadau mbalimbali katika tasnia ya burudani walihudhuria mazishi ya msanii huyo kutoka kundi la TMK Wanaume Family.
Mungu ailaze roho ya marehemu YP mahala pema Peponi. Amen.
Post a Comment