Taarifa iliyonifikia hivi punde kupitia Radio One Breaking News
inahusu kuuawa kwa mtuhumiwa namba moja wa kesi ya ulipuaji mabomu
jijini Arusha, Yahaya Hassan Omar kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi
la polisi wakati alipojaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi.
Tumekuwa tukipata taarifa zinazohusu matukio ya mauaji ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara nchini Tanzania, hali ambayo imeonekana kukithiri katika siku za usoni huku jeshi la polisi likitoa ahadi ya kufanya jitihada za kuhakikisha linawatia nguvuni wahusika wa matukio hayo.
Post a Comment