Msanii wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amemtaka msanii mwenzake, Jacqueline Wolper apime Ukimwi kama alivyofanya yeye.
Akiongea na mwandishi wetu, Rayuu alisema anamheshimu Wolper na
kamwe hawezi kumsema vibaya lakini alishangaa kuambiwa na mashosti wake
kwamba anamsema yeye ana Ukimwi.
“Nilishangaa sana kwa kweli hilo jambo liliniumiza roho na linaniuma
mpaka kesho, eti anawaambia watu mimi ni muathirika, lini alinipima au
ana uthibitisho gani na hilo,” alisema Rayuu na kuongeza:
“Kutokana
na kunikosesha raha kwa kiasi kikubwa kwa jambo hilo, niliangua kilio
nikaamua kwenda kupima na kuyaanika majibu yangu kwenye Istagram ili
aumbuke kwa kuwa nipo safi, kama na yeye anaweza, akapime tuone majibu
yake.”
Post a Comment