Msanii
TI akiingia katika Ukumbi wa Bongoyo uliopo katika Hoteli ya Sea Cliff
Jijini Dar Es Salaam kwaajili ya kufanya mkutano na waandishi wa Habari
kabla ya kupanda kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta muda mfupi ujao
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Bw Steve Ganon akiongea na
wanahabari leo katika ukumbi wa mikutano wa Bongoyo uliopo katika Hoteli
ya Sea Cliff Jijini Dar wakati timu nzima ya Serengeti na Prime Time
Promotions ambao ndio waandaaji wa Tamasha la Fiesta walipokuwa
wakimtambulisha msanii nguli kutoka Nchini Marekani TI kabla ya kupanda
jukwaani Muda mfupi ujao katika Viwanja vya Leaders.
Mkurugenzi
wa Clouds Media Group, Bw Joseph Kusaga akitoa machache kabla ya
kumtambulisha Msanii wa Muziki Kutoka Nchini Marekani TI ambae atapanda
kwenye jukwaa la Fiesta muda mfupi ujao katika Viwanja vya Leaders.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Ephraim Mafuru akitoa machache
wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya
Sea Cliff jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya wasanii kutoka mataifa mbalimbali ambao watapanda katika jukwaa la Serengeti Fiesta leo
Msanii
kutoka nchini Nigeria Davido akiongelea jinsi atakavyo wapagawisha
watanzania leo katika jukwaa la Serengeti Fiesta muda mchache ujao
katika viwanja vya Leaders.
Kijana wa Kitanzania ambae amemchora TI katika taswira ya Kimasai na kumkabidhi msanii TI kama Zawadi kutoka Tanzania
Wanahabari
wakiwajibika wakati wa mkutano wa Kumtambulisha Msanii TI ambae
atapanda katika jukwaa la Serengeti Fiesta leo katika Viwanja vya
Leaders.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Post a Comment