TAMKO LA WAKRISTO
BUKOBA KUHUSIANA NA MAUAJI PAMOJA NA UCHOMAJI MAKANISA TAREHE 11/10/2014.
--
Baada ya tukio la kutisha la kushambuliwa kwa washirika na
hatimaye kuuawa kwa mshirika na kujeruhiwa vibaya kwa mwingine kanisani Kagemu
PAG; Wachungaji na viongozi wa kiroho wa Bukoba tumepokea taarifa hizi kwa
mshtuko mkubwa. Tumekutana tarehe 10 Oct 2014 na kutafakari hatima ya wakristo
katika eneo hili.
1. Kanisa
la Living water pale Buyekera mlimani limechomwa moto mara
2. Kanisa
la Hofan ministries limechomwa moto pale Rugambwa.
3. Kanisa
la la International assemblies of God lilipo Magoti lilichomwa moto na
kuteketea.
4. Kanisa
la TAG Kihwa lilichomwa moto na kuteketea
5. Makanisa
mengine maeneo ya vijijini kuchomwa moto nayo ni pamoja na Ruhanga TAG, Kakindo
PAG na Kasharu EAGT.
6. Vitisho
na Kushambuliwa kwa mawe wakati ibada zikiendelea mara kwa mara Kanisa la PAG
Buyekera.
7. Kanisa
la EAGT Kibeta kushambuliwa kwa mawe baada ya kundi la watu kuvamia kanisani
miezi 3 iliyopita
8. Kanisa
la Harvest kushambuliwa kwa mawe usiku na kundi la watu.
9. Jaribio
la kuchomwa kisu Askofu Sesse Lazaro wakati akiwa kanisani.
10. Kifo
cha kutatanisha cha Mch Jackson Kabuga wa TAG Kashabo.
Mengi ya matukio haya yameripotiwa
katika vyombo vya usalama ingawa hatujapata mrejesho wowote toka vyombo hivi.
Kwa mtazamo wetu huu ni mpango
uliolasimishwa wa kujenga hofu na hatimaye kukomesha uhuru wetu katika
kumwabudu Mungu. Matukio haya japo yanaonekana hayahusiani lakini yamebeba
maudhui inayofanana na yanatekelezwa kwa mbinu zinazofanana na inawezekana na
kundi moja lenye mtandao mpana.
Kwa tamko hili tunataka yafuatayo
yazingatiwe:
a. Kwa
hali hii wakristo tutaweka mtandao unaojitegemea wa ki ulinzi wa nyumba za
ibada, viongozi wa kiroho, na washirika wetu pamoja na hatua nyingine zozote za
kiusalama tutakazoona zinafaa.
b. Tunaitaka
serkali ifanye uchunguzi wa kina juu ya tukio hili na mengine yaliyotangulia na
kutupatia taarifa ndani ya muda mfupi juu ya mafanikio au kukwama kwa
uchunguzi.
c.
Kwa wakristo wote walioguswa na kuumizwa na
tukio hili maneno la Mungu toka Rumi 8:37-39 yawe faraja yetu:
“Lakini katika mambo hayo yote
tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha
kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye
mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho
chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana
wetu.” Amen
Tamko hili limetolewa na
wachungaji 35 waliokaa katika kikao cha dhararula PAG tarehe 10/10/2014 na
kutiwa sahihi kwa niaba yao na:-
Mch Crodward Edward.
Mwenyekiti wa Umoja wa wachungaji
Bukoba.
Post a Comment