HESHIMA! Tofauti na ilivyokuwa ikifikiriwa na wengi kwamba hamkubali
shemeji yake, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameonyesha
kumkubali shemeji yake Ahmed Hashimu ‘Petit Man’ hadharani.
Shemeji wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ Ahmed Hashimu
‘Petit Man’ akiwa na 'waifu tu bi'.Hivi karibuni uvumi uliibuka kuwa
Diamond hakufurahishwa na kitendo cha dada’ke kuolewa na Petit ndipo
msanii huyo alipoamua kukata ‘vilimilimi’ kwa kusema uvumi huo hauna
ukweli katika sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika Oktoba 2, mwaka huu
kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee Tower, Posta jijini Dar.
“Kwa bahati mbaya dada yangu Esma anaumwa hajafika humu ndani, sasa
kwa kuwa sasa hivi ameolewa na mtu ninayemkubali, namuita mumewe,
shemeji yangu ninayemkubali, Petit Man aje kula keki badala yake,”
alisikika Diamond.
Post a Comment