Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZIRI MKUU PINDA ATEMBELEA KIWANDA CHA TREKTA POLAND

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda atatuma wataalamu wa sekta ya kilimo ili waje kufuatilia suala la mahitaji ya trekta ili kuziba pengo la mahitaji yake nchini Tanzania. Alisema lengo la Serikali la kuanzisha sera ya Kilimo Kwanza lilikuwa ni kuwasaidia wakulima kupata ruzuku ya pembejeo, mbegu bora, na dawa za mifugo ili waweze kuongeza ushalishaji.


“Kutokana na mkopo wa Serikali ya India, tulipata matrekta 1,846 ambayo hayakuchukua muda kuisha. Sasa hivi tunatafuta wabia wengine wa kutupatia zana za kisasa za kilimo kwa sababu matunda yake mazuri tumeyaona, tunataka kilimo cha Mtanzania,” alisema.

Jana asubuhi (Ijumaa, Oktoba 24, 2014), Waziri Mkuu alitembelea kampuni ya Farmers inayotengeneza vipuri pamoja na matrekta ya kulimia na kuvuna yenye ukubwa wa Horse Power 80 na 72 ambayo alielezwa kwamba yanavumilia hali ya udongo mgumu wa Afrika.

Akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Farmer, Bw. ZDZISLAW ZUKIEWICZ alisema vifaa vinavyotengenezwa na kampuni hiyo vina waranti ya miaka saba na vinaweza kuhimili udongo wa miamba na mawe wa ardhi ya Tanzania.

Kampuni hiyo inatengeneza matrekta, mashine za kuvuna mazao shambani (combined harvester), mashine za kukata nyasi za malisho ya mifugo pamoja na vipuri vyake. Alisema bei ya trekta ni wastani wa Euro 22,000 na wako tayari kuleta vifaa hivyo Tanzania kama watapewa oda.

Waziri Mkuu amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini Poland jana mchana ambapo asubuhi alikutana na Watanzania waishio Poland na baadaye kufanya vikao na baadhi ya wafanyabiashara wa jiji la Warsaw.

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, OKTOBA 26, 2014
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top