Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wema Sepetu: Najuta Kuwa Maarufu



‘BEAUTIFUL Onyinye’, WEMA Isaack Sepetu ‘Madame’ ametoa ya moyoni na kufichua kwamba maisha yake ya umaarufu anayoishi yanamtesa kwa asilimia 40.
Pamoja na mateso hayo, staa huyo wa filamu alisema anafurahia maisha yake kama mtu maarufu ikiwamo na kuandikwa na vyombo vya habari mara kwa mara.
“Kuna wakati najutia kuwa maarufu kwa asilimia kama 40 hivi lakini nashukuru kwani kwa asilimia 60 nayafurahia maisha yangu.
“Ukiwa nyota kuna changamoto nyingi sana, kuna wakati mtu anaweza kukuandika habari inayokufanya ushindwe hata kutoka nje na kubaki ndani tu,”alisema.
Wema alisema kuna wakati huwa anatamani asingekuwa maarufu kwani akifanya kitu kidogo hata kama ni cha kawaida lakini hupokelewa kama habari kubwa na kuongelewa sana.
“Lakini katika maisha kama haya sina cha kufanya japo kuna mambo ambayo huniumiza na najitahidi sana kuvumilia,” alisema.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top