Wananchi
wapatao 350 waliokuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kijiji cha
Msange, Jimbo la Singida Kaskazini, Wilaya ya Singida Vijijini, mkoani
Singida wakiwa wameshika kadi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) huku wakila kiapo cha uzalendo baada ya kujiunga na chama
hicho kwenye moja ya mikutano ya 'Operesheni Delete CCM' uliohutubiwa na
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zanzibar, Salum Mwalimu, mwishoni mwa
wiki.
Sehemu
ya Umati Mkubwa Ukimsikiliza Mwenyekiti Taifa wa Taifa wa Chadema
Freeman Mbowe alipohutubia mikutano mitano kwenye majimbo matatu ya
Ulanga Magharibi, Ulanga Mashariki na Kilombero.Mikutano yote ilikuwa
mikubwa sana na yenye hamasa kubwa huku wenyeviti saba wa CCM wa vijiji
kwenye jimbo la Ulanga Mashariki wakirudisha kadi za CCM na kujiunga na
CHADEMA na kuahidi kuongeza nguvu zaidi kwenye Operation Delete CCM
ambapo watasaidia wagombea watakao simamishwa na Chadema pamoja na vyama
vingine vya UKAWA.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman
Mbowe akiwahutubia wanachi wa kijiji cha Nyandila kilichopo juu ya
milima ya Uruguru mkoani Morogoro, katika mkutano wa hadhara wa
Oparesheni Delete CCM juzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman
Mbowe akiwahutubia maelfu ya wananchi wa mji wa Mtibwa katika jimbo la
Mvomero mkoani Morogoro, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni Delete
CCM juzi
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman
Mbowe akilakiwa na wanachi wa mji wa Gairo mkoani Morgoro baada ya
kuwasili, ambako alifanya mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM
juzi.
![](//2.bp.blogspot.com/-4B-b1eyeETk/VHIGYnmr4bI/AAAAAAADItg/ZZH8I1RHpGU/s1600/IMG_1208.JPG)
Naibu
Katibu Mkuu wa Chadema, Zanzibar, Salum Mwalimu akiwalisha kiapo cha
uzalendo wanachama wapya katika Kijiji cha Msange, Jimbo la Singida
Kaskazini, Wilaya ya Singida Vijijini, mkoani Singida waliohama kutoka
Chama Cha Mapinduzi, katika moja ya mikutano 'Operesheni Delete CCM',
uliofanyika mwishoni mwa wiki kijijini hapo,Picha na Chadema
on Tuesday, November 25, 2014
Post a Comment