Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Seif
Shaban Mohamed, amewataka viongozi wa jumuia hiyo kuwa wabunifu wa
miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuifanya jumuia hiyo kukua kiuchumi.
Mohammed ametoa agizo hilo leo, wakati akizindua Daftari la Wanachama
wa Jumuia hiyo Mkoa wa Dar es Salaam, hafla iliyofanyika katika ukumbi
wa Arnatouglou, mkoani humo.
“Nawapongezeni kwa kuunda kamati ndogondogo ndani ya jumuia, kufanya
hivi kuutasaidia kusogeza huduma kwa wanachama wetu na wananchi kwa
ujumla hivyo kukifanya chama chetu kiendelee kuaminiwa” alisema Mohamed.
Alisema Jumuia inazo rasimali nyingi hivyo ni vizuri sasa zikatumika
ipasavyo kukuza uchumi wa jumuia ya Wazazi na viongozi wa jumuia
wasipende kusubiri kila kitu muelekezwe na viiongozi wa juu.
Alitoa mfano wa kitegauchumi cha Jumuia hiyo kilichotelekezwa bila
kuendelezwa kuwa nieneo la shule ya jumuia hiyo ya Boza iliyopo mkoani
Tanga, ambapo alisema kuwa ina ardhi ya kutosha lakini haifanyiwi
uzalishaji mali wowote.
Mohamed alipongeza Jumuia hiyo Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanzisha
daftari hilo la wanachama akisema litasaidia kuwatambua wanachama wao
kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa hivyo kurahisisha shughuli za kisiasa
kwa kutambuana katika chaguzi mbalimbali na shughuli nyingine kama za
maendeleo.
Katika hatua nyingine Mohamed alisema wanajumuia wote ya wazazi
wanaiunga mkono Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalumu la Katiba na
kuwa wao wanautaka muundo wa serikali mbili kwani ndio utalipeleka mbele
Taifa la Tanzania.
Alitoa mwito kwa wanachama wote wa CCM kujitokeza kwa wingi kupiga
kura ya kuwachagua viongozi wao kuanzia ngazi za mashina wakati wa
uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika hivi karibuni.
Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Cholaje Ali, alisema mpango wa kuanzisha daftari hilo ni moja ya mikakati yao ya kuibadilisha jumuia kiutendaji.
Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Cholaje Ali, alisema mpango wa kuanzisha daftari hilo ni moja ya mikakati yao ya kuibadilisha jumuia kiutendaji.
“Hii jumuia yetu kwa muda mrefu ilikuwa nyuma kimaendeleo lakini
tumedhamiria kuibadilisha na kuwa ya kiutendaji zaidi na ndio maanna
tumeanzisha kamati ndogo ndogo za maendeleo na kuwateua watu wenye sifa
za kuziongoza yaani wenye taaluma” alisema Cholaje
Aliwataka viongozi wote waliochaguliwa kujitambua kuwa wamechaguliwa
si kwa bahati mbaya bali ni kwa ajili ya kuonekana kuwa wana uwezo wa
kuleta maendeleo ndani ya jumuia hiyo.
Post a Comment