Makamu wa Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Matamela Cyril Ramaphosa
akiteremka katika ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mhe. Ramaphosa
yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja ambapo pamoja na mambo
mengine atazungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano , Mhe. Stephen Wasira kwa
pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt.
Mahadhi Juma Maalim (Mb), na Bi. Zuhura Bundala, Kaimu Mkurugenzi wa
Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa wakati wa mapokezi ya Makamu wa Rais wa Afrika Kusini.
Mhe. Ramaphosa akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika mara baada ya kuwasili.
Mhe. Ramaphosa akisalimiana na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Talha Mohammed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akimkaribisha Ikulu Makamu wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril
Ramaphosa Matamela alipofika Ikulu kwa mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akizungumza na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Ramaphosa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa, Mhe. Bernard K.
Membe (Mb) kwa pamoja na Mhe. Wasira wakifuatilia mazungumzo kati ya
Mhe. Rais na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini (hawapo pichani)
Mazungumzo yakiendelea. Kulia ni Mhe. Radhia Msuya, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini
Picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mazungumzo.Picha na Reginald Philip
Post a Comment