Ama
kweli duniani kuna mengi,hii imetokea huko nchini Uganda baada ya mwanamke mmoja
mwenye watoto watatu katika Wilaya ya Kole nchini kumwandalia mumewe mlo wa
mipira ya kiume ya kondomu kufuatia ugomvi usiokwisha baina yao.
Maamuzi ya mwanamama huyu yanaweza kukushangaza sana
kwani pamoja na familia za wanandoa wengi kuwa na kawaida ya kutofautiana
wakati mwingine ni nadra sana kuona maamuzi yanayofanana na haya yakitolewa.
Kwa mujibu wa Gazeti la Daily Monitor mwanamke huyo
aliripotiwa kununua paketi tatu za kondomu aina ya Trust kutoka duka la jirani
kabla ya kuzipika na kumwandalia mumewe kama chakula baada ya kurudi nyumbani
akiwa amelewa chakari.
Baada ya kununua alirejea nyumbani na aliikatakata mipira
hiyo ambayo ilikua haijatumika katika vipande vidogo na kisha kuvichemsha
kwa muda na baadaye kukaanga na mafuta pamoja na viungo vingine na kumpa mumewe
ambaye licha ya ulevi wake alibaini chakula kilikua na ladha tofauti.
Hata
hivyo mwanamke huyo alisema alilenga kumfunza mumewe adabu kutokana na tabia
yake hiyo inayomkera ya kurudi nyumbani akiwa amechelewa na amelewa sana
Post a Comment