
Mtangazaji mahiri Gardner.G. Habash,amejiunga na kituo cha Radio
kinachokuja kwa kasi hivi sasa EFM 93.7 cha jijini Dsm ili kuongeza
nguvu katika kikosi chao.Akizungumza leo na waandishi wa habari afisa
habari wa EFM Kanky Mwaigomole amesema wameamua kumchukua Gardner
kwasababu ni miongoni mwa watangazaji hodari nchini mwenye kipaji cha
hali ya juu hivyo kuongeza chachu ya mafanikio katika kituo hicho
kipya.“Gardner ataendesha kipindi kiitwacho Ubaoni kuanzia saa tisa
alasiri mpaka saa moja kamili jioni kuanzia Jumatatu ya tarehe 03 mwezi
wa 11 mwaka huu”alisema Kanky
Post a Comment