Mwanamuziki huyo kaingia kwenye orodha ya mastaa wanaoelekea kubadilisha status zao baada ya kuvalishwa pete ya uchumba.
Nyota Ndogo ambaye jina lake halisi ni
Mwanaisha Abdalla amevalishwa pete hiyo na Henning Neilsen raia wa
Denmark baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa zaidi ya miezi tisa.
Nyota Ndogo amesema ameamka asubuhi na
kuvalishwa pete hiyo, anamshukuru Mungu kwa hilo kwani mpenzi wake
hampendi yeye peke yake bali anawapenda na watoto wake wawili na
anatarajia ndoa yake itakuwa ya kawaida ambayo watu wachache watakaopata
nafasi ya kuhudhuria ikiwemo ndugu na marafiki wachache.
Post a Comment