Mshindi
wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika BBC mwaka huu amepatikana. Baada ya
maelfu ya kura kuhesabiwa, mchezaji wa Algeria na nyota wa Porto, Yacine
Brahimi ndiye mshindi wa mwaka huu.
Hapajawahi
kutokea katika miaka 23 ya historia ya shindano hilo kwa mchezaji bora
kutoka Algeria kuishinda, lakini Brahimi amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo
baada ya mwaka uliokuwa na mbwembwe wa 2014.
Aliingiza
bao la ushindi dhidi ya mabingwa wa Hispania Barcelona, bao lengine la
kisasa katika ligi ya mabingwa wa ulaya na kisha kuwa katika msitari wa
mbele wakati nchi yake iliposonga mbele katika michuano ya kombe la
dunia.
Yacine BrahimiHio ilikuwa historia kwa Algeria kufika katika awamu ya muondoano katika dimba hilo.
Hii bila
shaka ilikuwa nafasi nzuri kwa mashabiki wa BBC pamoja na wapenzi wa
soka kumchagua kama mchezaji bora zaidi wa Afrika mwaka huu.
Aliwapiku
wachezaji wengine nyota wakiwemo, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon,
Vincent Enyeama wa Nigeria, Gervinho wa Ivory Coast na hatimaye Yaya
Toure - aliyenyakua ushindi mwaka jana.
Post a Comment