SHIRIKA LA USAFIRI DAR ES SALAAM (UDA)
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MADEREVA
SHIRIKA
la Usafiri Dar es Salaam (UDA) linawatangazia Watanzania wote kwamba
linahitaji kuajiri madereva kwa ajili ya kuendesha mabasi yake hapa
jijini
Waombaji
wa kazi ya udereva wanatakiwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 30-55,
ujuzi wa udereva wa mabasi kutoka katika vyuo vya VETA, NIT, au chuo
kingine kinachotambulika na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi nchini (NECTA).
Pia wanapaswa kuwa na leseni ya udereva daraja C Kavu (Class C Plain) na
daraja C1(Class C1) , rekodi nzuri ya utendaji na afya njema.
STAHILI
Waombaji
watakaochaguliwa watalipwa mshahara mnono wa kiasi cha Sh. 250,000/=
kwa mwezi, na pia watapatiwa matibabu bure wao na familia zao kupitia
mfuko wa bima ya afya.
NAMNA YA KUOMBA
Waombaji
wote walete barua zao za maombi wakiambatanisha na barua za udhamini,
walete barua hizo kwa mkono katika Ofisi ya Afisa Rasilimali watu na
Utawala, Makao Makuu ya UDA, KAMATA COMPLEX, mahali zilipokuwa ofisi za
mabasi ya SCANDINAVIA.
Wanawake wanye sifa wanahimizwa zaidi kuomba.
KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA
NAMBA 255222127421, 0766777754, 0766777753 ,0754776700,0715776500,0712000037 au wasiliana kwa barua pepe info@uda.co.tz, uda@umojainvestments.com au kwa sanduku la posta
Shirika la Usafiri Dar Es Salaam (UDA)
S.L.P 872
Dar Es Salaam,Tanzania
LIMETOLEWA NA OFISI YA MAHUSIANO YA UMMA
DESEMBA 01, 2014.
Post a Comment