Wakati wa kufungua mwaka, mfalme wa taarab Mzee Yussuf akaamua kubadili usafiri wake kwa kuachana na Toyota Ipsum na kununua Toyota Harrier (pichani juu) yenye thamani ya milioni 35.
Gari hilo bab kubwa likaingia kwenye mitandao ya kijamii, wengi wakimpongeza Mzee Yussuf huku wachache wakimpiga vijembe kwa madai ya kuwa yeye siyo msanii wa kwanza wa taarab kumiliki usafiri wa bei mbaya. Akatajwa Zuhura Shaaban mwenye kumiliki Hummer.
Lakini Mzee Yussuf ameiambia Saluti5 kuwa anayachukulia maneno hayo kama mambo ya kawaida kutoka kwa walimwengu na kwamba hafanyi maisha yake kwaajili ya kushindana na mtu bali ni kwa manufaa yake na familia yake.
“Nimekuwa nikibadili usafiri mara kwa mara, namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kupata gari la ndoto yangu, sijui kesho au kesho kutwa panapo majaaliwa nitatamani au nitamiliki gari gani, Mungu ndo anajua,” alisema Mzee Yussuf.
“Haya ni maisha ya kawaida, kila mtu ana njozi zake na mipango yake, sifanyi kitu kwa kushindana na mtu bali natii kiu yangu,” aliongeza Mzee Yussuf.
Hata hivyo wakati watu wakiitolea macho Harrier ya Mzee Yussuf, Saluti5 imebaini kuwa msanii huyo anamiliki malori mawili (tipa) aina ya Scania ambayo yako Chanika yakifanya kazi kwenye kampuni yake ya uuzaji na usambazaji wa vifaa vya ujenzi.
Ni gari za bei mbaya - ukizilinganisha thamani yake na Toyota Harrier ni sawa na kichuguu na mlima. Huyo ndo Mfalme Mzee Yussuf.
Gari la Mzee Yussuf linavyoonekana kwa ndani
Gari la Mzee Yussuf linavyoonekana kwa nje
Sehemu ya ndani ya gari hilo upande wa mbele
Kitu kimetulia
Likiwa limebaki mbele ya ofisi za Saluti5 Kinondoni jijini Dar es Salaam
Hakika ni gari la starehe
Mzee Yussuf akiwa ametulia ndani ya mchuma wake
Moja ya Scania anazozimiliki Mzee Yussuf
Post a Comment