|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini
Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Zambia kwa
ajili ya mazungumzo rasmi na Mwenyeji wake Rais Edgar Lungu ( mwenye
suti ya kijivu aliyesimama mbele ya Rais Kikwete) |
|
Rais Lungu akimkaribisha Rais Kikwete (hayupo pichani kuzungumza) |
|
Mhe.
Rais Kikwete akizungumza wakati wa mazungumzo rasmi na Rais Lungu na
Ujumbe wake katika Ikulu ya Zambia. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Mebe na kulia ni Waziri wa
Fedha, Mhe. Saada Mkuya Salu na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe.
Grace Mujuma. |
|
Mazungumzo yakiendelea |
|
Sehemu
nyingine ya ujumbe wa Tanzania wakati wa mazungumzo rasmi akiwemo Mhe.
Charles Tizeba (wa kwanza kulia), Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Abbas
Kandoro (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bi. Zuhura Bundala (wa
tatu kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bi. Talha Mohammed (wa
kwanza kushoto), Afisa Mambo ya Nje. |
|
Picha ya Pamoja |
|
Mhe. Rais Lungu akiwa amefuatana na Mhe. Membe.
==============================================
Tanzania
na Zambia zimekubaliana kushirikiana na kuimarisha sekta ya miundombinu
hususan kufufua Reli inayounganisha nchi hizi mbili (TAZARA) ili kukuza
biashara na uwekezaji.
Makubaliano hayo yamefikiwa jana wakati wa ziara ya siku mbili ya Rais wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete nchini Zambia.
Akizungumza
wakati wa mkutano rasmi kati yake na mwenyeji wake, Mhe. Edgar Lungu,
Rais wa Zambia, Rais Kikwete alisema kuwa umefika wakati sasa wa
kuifufuA Reli ya TAZARA ambayo ni kiungo muhimu na alama kubwa ya
ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia.
Mhe.
Rais Kikwete alifafanua kuwa umuhimu wa reli hiyo ni wa kihistoria
ambao unahusisha nchi tatu za Tanzania, Zambia na Jamhuri ya Watu wa
China ambao kwa kiasi kikubwa walichangia ujenzi wa reli hiyo.
“Upo
umuhimu mkubwa wa kuifufua Reli ya TAZARA ili ifanye kazi kama awali
kwani ni alama na kiungo muhimu cha ushirikiano wetu sisi Tanzania na
Zambia”, alisema Rais Kikwete.
Aidha,
aliongeza kuwa Tanzania na Zambia zimekubaliana kuwekeza zaidi katika
reli hiyo ikiwemo kuboresha uendeshaji na ukarabati ili kuirejesha
katika hali yake ya awali na hatimaye kukuza biashara na uwekezaji.
Alifafanua
kwamba hapo awali reli hiyo iliweza kusafirisha tani zaidi ya milioni 2
za bidhaa kwa mwaka wakati sasa reli hiyo inasafirisha tani laki 2 kwa
safari inayotumia hadi siku 12 kutoka Dar es Salaam hadi New Kapiri
Mposhi wakati malori yanatumia siku tano pekee.
“TAZARA
inapita katika kipindi kigumu sasa, hivyo tumezungumza namna ya kutatua
changamoto mbalimbali zinazoikabili ikiwemo uendeshaji na ukarabati ili
irejee katika hali yake ya awali”, alisisitiza Rais Kikwete.
Katika
hatua nyingine Mhe. Rais Kikwete alimpongeza Rais Lungu kwa kuchaguliwa
hivi karibuni kuwa Rais wa Zambia na pia alitoa salamu za pole kwa Rais
huyo na Wazambia wote kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa nchi hiyo,
Hayati Michael Satta.
Kwa
upande wake, Rais Lungu alisema kuwa Tanzania na Zambia zinajivunia
mafanikio ya ushirikiano yaliyopo baina ya nchi hizi mbili ambayo
yamejikita katika sekta za Kilimo, Usafirishaji, Nishati na Mawasiliano.
Pia,
alisema kwamba nchi yake ipo tayari kuimarisha ushirikiano wa
kihistoria uliopo ambao unaanzia ngazi ya serikali, kanda, Bara na
Kimataifa na kusisitiza umuhimu wa kuitumia Tume ya Kudumu ya Pamoja ya
Ushirikiano (JPC) ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 1992 kwa ajili ya
kusimamia utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yanayofikiwa na nchi
hizi mbili. Aidha, alikubaliana na hoja ya kuifufua reli ya TAZARA kwa
manufaa ya nchi hizi mbili.
Rais
Kikwete ambaye alikuwa nchini humo kwa mwaliko wa Rais Lungu alifuatana
na Mama Salma Kikwete, Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Saada Mkuya Salum, Waziri wa Fedha, Mhe.
Dkt. Charles Tizeba, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Abbas Kandoro, Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Grace Mujuma, Balozi wa Tanzania nchini Zambia na
Viongozi Waandamizi kutoka Serikalini na Mamlaka mbalimbali.
|
on Thursday, February 26, 2015
Post a Comment