Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya AS Monaco wakiwa ugenini. Lakini wametolewa na kushindwa kusonga katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kilichowang’oa Arsenal ni kupoteza kwa mabao 3-1 katika mechi ya kwanza wakiwa nyumbani Emirates, London.Olvier Giroud na Aaron Ramsey aliyeingia kipindi cha pili ndiyo waliofunga mabao hayo mawili.Juhudi za Arsenal kusaka bao moja litakalowavusha zilishindikana.Monaco licha ya kuwa nyumbani, walishindwa kucheza kwa kiwango kizuri cha ushindani. Hata hivyo, Arsenal hawakuwa katika kiwango cha juu sana kushindwa kuupasua mfumo wa ulinzi wa Wafaransa hao.
Post a Comment