Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HATARI SANA: MCHINJAJI MAARUFU DUNIANI ALIVYOKAMATWA DAR


Jihadi John ‘Mohammed Emwazi’ (26).
Kwa wale wasiomfahamu sawasawa muuaji huyo, anaonekana mara kwa mara katika runinga akiwachinja bila huruma watu waliotekwa na kundi lake la IS. Wamarekani wanamsaka kila kukicha!
Sasa Mei 22, 2009, John akiwa na wenzake wawili walitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa lengo la kuingia nchini ambapo habari za ndani kutoka uwanjani hapo zinasema walikuwa wafikie Masaki kwa mwenyeji wao mmoja ambaye ni raia wa Yemen. 
Inadaiwa kuwa, John na wenzake walikuwa wamekuja nchini kwa utekelezaji wa mafunzo ya vitendo vya kigaidi nchini lakini azima yao hiyo ikaishia mikononi mwa askari wa Kituo cha Polisi Kikuu cha JNIA, Dar baada ya kubainika kuwa, walikuwa wamelewa tangu wakiwa ndani ya ndege.
Mohammed Emwazi akijiandaa kumchinja mateka.
Hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe amesema kuwa, John na marafiki zake hao walizuiwa kuingia nchini mwaka 2009 kwa sababu walikuwa wamelewa sana na kuwatukana maafisa wa uhamiaji wa uwanja huo.
Alisema John na wenzake walitua Dar saa 10 jioni wakiwa ndani ya ndege ya KLM kutoka Amsterdam (Uholanzi). Waziri Chikawe alisema rubani wa ndege hiyo ndiye aliyewataarifu maafisa wa uhamiaji hao kwamba kulikuwa na watu kwenye ndege wamelewa kupindukia. 
Habari nyingine zilidai kuwa, John na wenzake walikuwa waungane na mwenyeji wao kwa safari ya nchini Somalia ambako alitakiwa kwenda kuanza kuchinja wanajeshi wanaoisaidia serikali ya nchi hiyo. 
Hata hivyo, habari nyingine zinadai kuwa, mwenyeji wao huyo alikimbia nchini baada ya kuhisi kusakwa na maafisa usalama huku akienda kuwashitaki John na wenzake kwa kulewa kupita kiasi huku wakijua walikuwa na kazi nzito mbele yao. 

Katika kituo hicho cha polisi uwanja wa ndege, John na wenzake walilala kwa siku moja kabla ya kurudishwa walikotoka huku baadhi ya maofisa wakiambiwa na mahabusu kuwa, John na wenzake walikuwa wakizungumzia mambo ya mauaji kwa muda mrefu
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top