Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
IMEVUJA! Ile mimba ya aliyekuwa Mtangazaji wa Efm Radio, Penieli Mungilwa ‘Penny’ ambayo ilijulikana alipachikwa na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ imezua mzozo upya baada ya kuvuja kwa madai mengine. Chanzo makini kimeliambia Amani kwamba, tofauti na madai ya Diamond kwamba Penny alitoa mimba yake, lakini kumbe Diamond hakumpa mimba ila ilikuwa ni magumashi ya Penny.“Hali ilikuwa hivi! Kutokana na Diamond kutafuta mtoto kwa muda mrefu, hasa kwa mpenzi wake wa nyuma Wema Sepetu kushindikana, ikabidi Penny atumie mbinu yake ili kufaidika na pesa za Diamond.“Penny aliahidiwa na Diamond kwamba, kama atakubali kuzaa naye atamnunulia gari zuri, kwa hiyo kazi ikawa kwa Penny sasa, afanyaje?
“Siku moja Penny alimwambia Diamond kwamba amenasa, Diamond akafurahi sana, lakini kumbe Penny alishaenda kwenye hospitali moja kubwa iliyopo Kinondoni (jina tunalo), akaongea na nesi mmoja kwamba kama atakwenda na Diamond kupima mimba akubali kwamba anayo, lengo lake ni kupata gari,” kilisema chanzo hicho.SOMA ZAIDI>>>
Mtangazaji wa Efm Radio, Penieli Mungilwa ‘Penny’ akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond’.
IKAZIDI KUDAIWAChanzo kikazidi kudai kwamba, ili amridhishe Diamond, Penny alimchukua mpenzi wake huyo hadi kwenye hospitali hiyo na kukutana na yule nesi ambaye alimwambia Diamond kwamba kweli mchumba wake huyo (kwa wakati ule) alikuwa amenasa.“Ndipo Diamond ikabidi amnunulie gari Penny aina ya Toyota Brevs la rangi ya bluu iliyoiva. Siku mbili tatu, akageuka, akamwambia Diamond mimba imetoka, ndiyo kikawa kisa cha kumwagana,” kiliongeza chanzo chetu.
PENNY ASAKWA NA AMANI
Baada ya kupata madai hayo mazito, Amani lilimvutia ‘waya’ Penny na kumsomea mashtaka yake ambapo alisema kuwa, hafikirii katika kumbukumbu zake kama alishawahi kusema yeye ni mjamzito au alikuwa na mimba ya Diamond kama siyo mwanamuziki huyo kutangaza mwenyewe.
“Hivi jamani! Mimi sijawahi kusema kama nina mimba ya Diamond hata siku moja, sasa hapo hushangai aliyekuwa akisema nina mimba ni Diamond na siyo mimi. Kwanza Diamond hajawahi kunipa mimba hata siku moja, muulizeni aseme ukweli wake. Kama ni gari ni mapenzi yake lakini si zawadi ya mimba,” alisema Penny.
‘Penny’ akiwa na mama Diamond.
DIAMOND NAYEKwa upande wake, Diamond alipoulizwa kuhusu madai ya kuingizwa mjini na Penny kuhusu mimba, alikuwa na haya ya kusema:“Mm! Hiyo kali zaidi! Mimi Penny aliponiambia ana mimba yangu, asubuhi nilimkurupua mwenyewe, nikampeleka kwenye hospitali yangu mimi, hakunipeleka yeye.
“Tena hakujua kama nampeleka hospitali gani. Kule daktari wangu akampima, akamuona amenasa kweli. Sasa mnaposema eti alinipeleka kwenye hosptali yake aliyokwishapanga na nesi, nashangaa, siyo kweli bwana.“Yeye kama alifanya hivyo labda alimfanyia mtu mwingine, si mimi. Sasa naona kama kuna mzozo unataka kuibuka upya hapa.”
PENNY, ARUDIWA, HAPOKEI SIMU
Jumatatu iliyopita, Penny akapigiwa simu tena ili kupewa majibu ya Diamond, lakini simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Lakini Amani linaendelea kumfuatilia ili kumsikia atasema nini kuhusu majibu ya Diamond.
Post a Comment