Pichani
Msafara wa Katibu Mkuu,Ndugu Abdulrahman Kinana ukielekea jimbo la
Kimbakwe Wilayani Mpwapwa mapema leo asubuhi kuendelea na ziara yake
ya siku 9 mkoani Dodoma ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua nakuhimiza
utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010 pamoja na kusikiliza kero za
Wananchi ikiwemo na kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na baadhi ya vijana waliopo
katika kituo cha mradi wa Wanyama kazi ndani ya kijiji cha
Kibakwe,wilayani Mpwapwa.
Mmoja
wa Vijana waliopo katika kituo cha mradi wa Wanyama kazi ndani ya
kijiji cha Kibakwe,wilayani Mpwapwa wakitoa maelezo mafupi mbele ya
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana namna zana hizo za kilimo zinavyotumiwa
na wanyaka katika suala zima la kilimo.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kuhusiana na uoteshaji
wa mbegu za miti ya mikorosho katika kituo cha mradi wa Wanyama kazi
ndani ya kijiji cha Kibakwe,wilayani Mpwapwa.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua shamba la mfano la Wanaushirika
waitwao Mkombozi,lililopo karibu na kituo cha mradi wa Wanyama kazi
ndani ya kijiji cha Kibakwe,wilayani Mpwapwa.
Mwenyekiti
wa kikundi cha Mkombozi,Bwa.Athanas Kigosi akitoa maelezo mafupi mbele
ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,kuhusiana na shamba la mfano ambalo
limepandwa mahindi,lililopo katika kijiji cha Kibakwe,Wilayani
Mpwapwa.Bwa.Athanas alieleza changamoto wazipatazo katika maandalizi yao
ya kilimo kuwa suala la pembejeo limekuwa tatizo kubwa kwao,kwani
zimekuwa zikiletwa kinyume na wakati,hali inayowapelekea ugumu
wa kuendelea na kilimo kwa wakati,mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo
sambamba na mazao yao kutopandishwa bei,Hivyo Bwana Athanas ameiomba
serikali kuwasaidia wakulima kupelekewa pembejeo kwa wakati ili
kuhakikisha maandalizi ya kilimo yanakwenda kwa wakati.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akifafanua jambo kwa Wanahabari katika shamba
la mfano ambalo limepandwa mahindi,lililopo katika kijiji cha
Kibakwe,Wilayani Mpwapwa.Pichani kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Taifa,Nape Nnauye.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa darasa la shule ya
sekondari Ikuyu katika kijiji cha Luhundwa,wilaya ya Mpwapwa.Ndugu
Kinana alikagua na kushiriki mradi wa ujenzi wa darasa la shule hiyo na
kuwasalimia wananchi.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha
Luhundwa mapema leo,alipokwenda kushiriki ujenzi wa darasa la shule ya
sekondari Ikuyu katika kijiji cha Luhundwa,wilaya ya Mpwapwa.
Wananchi
wa kata ya Rudi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mara
baada ya kukagua na kushiriki ujenzi wa ofisi ya Mtendaji Kata.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akishiriki mradi wa ujenzi wa ofisi ya
Mtendaji Kata ya Rudi,Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.Mwisho kulia ni
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma,Mh.Addam Kimbisha pamoja na Diwani wa
kata hiyo,Mh.Nyaulingo Bulamlete.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiweka jiwe la msingi katika ofisi ya CCM tawi la Mtamba,wilaya ya Mpwapwa.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye wakifurahia jambo mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika
ofisi ya CCM tawi la Mtamba,wilaya ya Mpwapwa.
Wakazi
wa jimbo la Kibakwe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye
uwanja wa Kibakwe stendi,Katibu Mkuu aliwataka viongozi wanaosimamia
sheria kuzingatia wananchi wa kawaida na kuwashirikisha kwenye jambo
linalowagusa kwenye shughuli zao za kila siku kwani kufanya hivyo
kutawasaidia wananchi hao kuishi maisha yao na pia kuinua uchumi wa eneo
husika.
Wakazi
wa jimbo la Kibakwe wakimshangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye uwanja wa Kibakwe stendi.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kibakwe
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Kibakwe wilayani
Mpwapwa.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa akihutubia wakazi wa
Kibakwe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Kibakwe na
kuwataka wana CCM kuchagua viongozi wanaowataka na kusema wilaya au mkoa
hawataka jina la mtu yeyote aliyechaguliwa na wananchi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati wa
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Stendi ya
Kibakwe,jimbo la Kibakwe wilaya ya Mpwapwa,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara
ya kujenga na kuimarisha chama mkoa wa Dodoma akiwa ameongozana na
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Wakazi
wa jimbo la Kibakwe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye
uwanja wa Kibakwe stendi,Katibu Mkuu aliwataka viongozi wanaosimamia
sheria kuzingatia wananchi wa kawaida na kuwashirikisha kwenye jambo
linalowagusa kwenye shughuli zao za kila siku kwani kufanya hivyo
kutawasaidia wananchi hao kuishi maisha yao na pia kuinua uchumi wa eneo
husika.
Post a Comment