UKARIBU wa mastaa wa filamu za Kibongo, Kulwa Kikumba maarufu kama Dude na msanii mwenzake Ester Kiama unaonyesha kama kuna kitu kati yao baada ya kuonekana kuwa karibu kwa muda mwingi kiasi kinachotia shaka!
Chanzo kilicho karibu na wawili hao kimesema mara kwa mara wanaonekana kuwa karibu kila wanapokwenda na kuonyesha dalili zote za kimahaba, lakini wenyewe wanadai ni washkaji walio kazini.
Gazeti hili lilibahatika kuwafuma wakiwa pamoja na walipoulizwa juu ya tuhuma za kujihusisha kimapenzi, kila mmoja alimtupia msalaba wa kujibu mwenzake. “Mh, jibu wewe, mimi najua Dude ni kaka yangu na ni mfanyakazi mwenzangu”, alisema Ester.
Post a Comment