Tumezoea kuona vijana au watu wa makamo kufunga ndoa lakini ilikuwa ajabu kwa vikongwe hawa kuchukua uamuzi huo wakiwa na umri mkubwa.
Vikongwe hao Dikam mwenye umri wa miaka 107 na Ka’a Nafung mwenye miaka 95 Nigeria wameamua kufunga ndoa huku wakiwashangaza watu kwa uamuzi wao huo kutokanana umri wao.
Imeelezwa kuwa ndoa hiyo ilifungwa
kutokana na kila mmoja mwenza wake kufariki dunia na kuwaacha wapekwe
hivyo kuamua kutafuta faraja na kukutana kisha kuamua kufunga ndoa.
Bibi harusi ana mtoto mwenye umri wa miaka 65 ambaye ndiye pekee aliyebakia baada ya wengine kufariki.
Ndoa hiyo ilifungwa katika kanisa la Christ in Nations (COCIN) ambapo watu wengi walifurika kushuhudia ndoa hiyo huku wakiwapongeza kwa hatua hiyo.
Akisimulia historia ya maisha yake bwana
harusi amesema alikuwa na wake saba na watoto 32 enzi za ujana wake,
wakati huo alikuwa hamtambui Mungu na alikuwa na maisha ya kuoa na
kuacha kila wakati.
Post a Comment