Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ZIARA YA KINANA WILAYA YA ARUMERU MAGHARIBI YAACHA GUMZO


 
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia)akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Ndugu Goodluck Ole Medeye mara baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Oldonyosambu.
 Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha Flora Lazari Zelothe akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Oldonyosambu wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM.
 Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Ndugu Goodluck Ole Medeye akisalimia wananchi wa kijiji cha Oldonyo Sambu waliojitokeza kumpokea  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha Chama.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa kijiji cha Oldonyosambu ambao walijitokeza kumpokea alipowasili kwenye jimbo la Arumeru Magharibi.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka kukagua daraja la Kisongo.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi kwa kupeleka zege kwenye eneo husika wakati wa ujenzi wa daraja la Kisongo.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa kata ya Kisongo mara baada ya kushiriki ujenzi wa daraja la Kisongo.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipandisha bendera ya shina la wakereketwa la Mateves kama ishara ya kufungua rasmi shina hilo.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nduruma ambao walikuwa na malalamiko juu ya mradi wa maji wa Nduruma kuonekana kupelekwa mashambani badala ya maeneo wanayoishi watu.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa kutoka wilaya ya Arumeru Magharibi Ndugu Mathias Manga wakati wakiwasili kata ya Mlangarini tayari kushiriki ujenzi wa Kituo cha Afya cha kijiji cha Manyire.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka zege wakati wa ujenzi wa kituo cha afya cha Manyire.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya jengo la kituo cha afya cha Manyire kutoka kwa MNEC Mathias Manga.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wazazi,walimu na wananchi waliojitokeza kumsikiliza alipotembelea shule ya Sekondari ya Sokon II
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi katika shule ya sekondari ya sokoni II.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa mkutano wa halmashauri kuu ya wilaya ya Arymeru Magharibi
 Wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya ya Arumeru Magharibi wakimsikiliza  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi akihutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya shule ya msingi Ngaramtoni,Arusha.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ngaramtoni ambapo alitoa sababu mbali mbali za dalili za kufa kwa upinzani nchini.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ndugu Onesmo Ole Nangole akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa CCM wilaya ya Arumeru Magharibi uliofanyika Ngaramtoni shule ya Msingi ambapo alitoa sifa kwa  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa kazi nzuri ya kuimarisha Chama.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ngaramtoni ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa CCM ya sasa haitofanya makosa, na kuwahakikishia kila atakayefanya makosa itabidi aubebe msalaba wake.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top