Kwa mujibu wa tovuti ya Bunge inayoonyesha idadi ya maswali yaliyoulizwa na michango ya kila mbunge, wapo wabunge wawili ambao hawajawahi kuuliza wala kuchangia chochote tangu Bunge hilo, lenye wabunge 358, lilipoanza Uchaguzi Mkuu uliopita hadi sasa.
Vilevile, tovuti hiyo inabainisha majina ya wabunge waliofanya vizuri zaidi katika kila eneo, yaani maswali ya msingi, ya nyongeza na michango waliyotoa katika mijadala mbalimbali.
Katika orodha hiyo, Spika Anne Makinda, ambaye pia ni mbunge wa Njombe Kusini, ndiye anayeonekana kinara kwa kuchangia mara 2,055 pale anapoongoza Bunge na kuuliza swali moja huku naibu wake, Job Ndugai akiwa amechangia mara 1,350 bila kuuliza swali hata moja.
Kiwango cha michango ya wabunge kimeelezwa na baadhi ya wasomi kuwa inategemea mambo mengi, ikiwamo mbunge kuwa sehemu ya Serikali na hivyo kushindwa kuihoji, uwezo wake kielimu na msimamo wake kiitikadi.
“Wabunge wengine tunaona ni wafanyabiashara ambao hawana elimu. Walishinda kwenye uchaguzi kutokana na fedha zao lakini hawana uelewa wa mambo..
Alisema orodha ya wabunge 10 waliochangia sana na wengine 10 waliochangia mara chache, haihusishi kiti cha spika, wenyeviti wa Bunge na mawaziri.
Wabunge 10 wenye michango michache
Nambari moja inashikwa na wabunge wawili ambao pia ni viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ambao ni mbunge kutoka Baraza la Wawakilishi, Mohamed Said Mohamed (CCM) ambaye ni mwakilishi wa Mpendae na Naibu Waziri wa Kilimo na Maliasili, pamoja na mbunge wa Kitope (CCM), Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Anayefuatia ni mbunge wa Babati Mjini, Kisyeri Chambiri (CCM) ambaye amechangia mara nne lakini hakuwahi kuuliza swali lolote.
Katika orodha hiyo wabunge waliochangia mara tano bila kuuliza maswali yoyote ni DkMohamed Seif Khatibu (Uzini – CCM), Edward Lowassa , Shawana Hassan (Dole – CCM). Mbunge wa Kalenga, Godfrey Mgimwa aliuliza maswali matatu ya nyongeza na kuchangia mara mbili.
Mwingine ni Ali Haji Juma wa (Chaani – CCM) aliyechangia mara nne, akauliza swali moja la msingi na moja la nyongeza.
CHANZO:MWANANCHI
Post a Comment