Mkutano wa 20 na wa mwisho wa Bunge la 10 ambalo litapitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2015/16 tayari umeanza mjini Dodoma asubuhi hii.
Wabunge watachangia bajeti za wizara na Bajeti Kuu ya Serikali ndani ya siku 44 ikilinganishwa na siku 56 zilizotumika kupitisha bajeti ya mwaka 2014/15 na miaka ya nyuma na bunge hilo litamalizika Juni 27.
Badala ya Bunge kuanza saa 3.00 asubuhi hadi saa 7.00 mchana na baadaye saa 11 jioni hadi saa 1.45 usiku kama ilivyokuwa hapo awali, kwa sasa litaanza 3.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana na kuendelea saa 10.00 jioni hadi saa 2.00 usiku ili kuendana na muda huo wa siku 44 badala ya 56.
Serikali imepanga kukusanya na kutumia Sh22.4 trilioni katika mwaka wa fedha 2015/16 ikiwa ni nyongeza ya Sh2.6 trilioni ikilinganishwa na Bajeti ya mwaka 2014/15 ambayo ilikuwa Sh19.8 trilioni.
Post a Comment