Mama mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja amefanya aibu
ya mwaka baada ya kusaula (kuvua) nguo zake na kubaki mtupu, kisa
kikidaiwa ni kumlaani ‘serengeti boy’ wake aliyemfanyia kitu mbaya.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mwanamke huyo mbali ya kuwa na mtu wake
amedaiwa kuwa na tabia ya kuchepuka na wanaume tofauti ambapo amekuwa
akifanya hivyo kwa kupanga chumba katika moja ya gesti
iliyopo Sinza kwa Remmy, jijini Dar.
Inadaiwa kuwa tukio hilo lililotokea hivi karibuni, mwanamke huyo
kama kawaida yake alipata mteja ambaye ni mdogo kwake kiumri, ambaye pia
ni mkazi wa eneo kulikotokea varangati hilo.
“Walikubaliana na huyo kijana kupumzika kwa muda na yule mwanamke
katika chumba alichopanga, baada ya kumaliza mambo yao kijana aligoma
kumpa hela ndipo mtiti ulipoanzia,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;
”Tulishangaa kuona watu wakivutana
huku mwanamke akiwa na kanga moja, ndipo kijana akapata upenyo na
kuchoropoka na mwanamke yule akaanza kuvua nguo huku akisema anamlaani
kutokana na umri wake kuwa mdogo na kumdhulumu chake.
“Watu walimsihi lakini akawa hasikii zaidi ya kuendelea kuvua na
kuamua kumfuata yule kijana kwao huku akiendelea kuvua njia nzima,
alipofika kwa yule kijana alianza kugonga geti kwa fujo huku akitoa
maneno ikiwemo ya kumlaani.
“Pamoja na makelele na kusaula kote nguo zake lakini hakuambulia kitu
zaidi ya kuonesha sehemu zake za siri na baadaye aliamua kuondoka."
Post a Comment