Baada ya wiki kadhaa
kupita tangu picha zake zisambae zikimuonesha gauni likiwa limevuka
nakuachia maziwa wazi, staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’
ameibuka na kuwaomba radhi kinamama wote.
Shilole
amesema kuwa anajua kwamba kitendo hicho kimewakwaza wengi na
hakukusudia kufanya jambo kama lile. “Nimejifunza mengi na naendelea tena kuomba msamaha kuwa tatizo hili halitajitokeza tena ,niwaombe radhi kina mama na mashabiki wangu,” alisema.
Shilole alifanya tukio hilo alipokuwa jijini Antwepen, Ubelgiji kwenye shoo ambapo aliongozana na mpenzi wake,Nuh Mziwanda
Post a Comment