Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu
-
“Nimesikitishwa sana na kauli ya Mhe. Joshua Nassari ambayo ameongea kwa kudhalilisha utendaji wangu serikalini. Naomba Mh. Nassari afahamu kuwa kunikashifu pasipo kueleza masuala ya kisera au ya kiutendaji ni kupungukiwa na busara ya kawaida kwa kiongozi aliyepaswa kuwawakilisha wapiga kura wake kwa hoja.
Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Mhe. Nassari aliniita Jimboni kwake Arumeru Mashariki akiniomba nitatue tatizo lililohusu wananchi wa jimboni kwake waliokuwa wanahitaji matibabu katika hospitali ambayo ilikuwa sharti upitie ndani ya hifadhi ili ufike kutibiwa. Nilikwenda kuwaona wagonjwa na kuitembelea hospitali hiyo na kulitatua tatizo hilo siku hiyo hiyo. Kwangu kama Waziri, halikuwa suala la kufanyia siasa afya za Watanzania, pamoja na yeye kuwa Mbunge wa upinzani. Nilimheshimu na kukubali wito wake kwa niaba ya wananchi.
Nimewatembelea na kuwatia moyo maaskari wetu nchi nzima na kuwapelekea vitendea kazi. Nimefurahi pamoja nao na kulia pamoja nao. Nimeenda kuwafariji familia za wapiganaji wetu waliopoteza maisha kwa kuuawa wakilinda raslimali za Taifa, watu ambao Mhe. Nassari anawabeza. Tumepambana na ujangili na tunaendelea kuushinda.
Tumeleta magari, silaha, ndege, helicopters, na raslimali nyingi ili kulinda raslimali za Taifa. Busara haisomewi ila ni kumshukuru Mungu akusaidie kujua matumizi ya ulimi. Nimesikitishwa sana na kauli za uongo na kuzusha za Mhe. Nassari. Imeandikwa, usimsingizie jirani yako uongo.”
Mh. Lazaro Nyalandu
Post a Comment