WATU wawili wamekamatwa katika vituo viwili tofauti vya uandikishwaji wa daftari la mpigakura kwa kosa la kuchana karatasi ya maelezo ya mpiga kura (Fomu namba moja) na mwingine kwa kosa la kujiandikisha mara mbili.
Akizungumza juzi na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Jiji la Arusha, Juma Idd, kuhusu matukio hayo,
yaliyotokea Jimbo la Arusha Mjini, alisema Fauzia Abdurai Mussa, ambaye
ni binti aliyekuwa amevaa vazi maalumu la hijab alifika kujiandikisha
fomu namba moja katika kituo cha YMCA kata ya Kati ambaye alipofika
katika eneo la kupiga picha alitakiwa kuvua hijabu ili sura ionekane
lakini alikataa.
“Lakini huyu binti alipolazimishwa kuvua vazi hilo alikataa na kutoka
nje, na alipofika nje alichana karatasi hiyo ambayo ndiyo fomu namba
moja yenye maelezo yake na hapo alikamatwa na askari kutokana na
uharibifu wa mali ya serikali na yupo ndani anasubiri kupelekwa
mahakamani Jumatatu,” alisema.
Mtuhumiwa wa pili aliyemtaja kuwa ni Daniel Leonard alikamatwa katika
kituo cha shule ya msingi Daraja mbili, kata ya Daraja mbili baada ya
kudaiwa kujiandikisha Julai 13 na Julai 15, mwaka huu katika kituo
hicho, hivyo alitiwa mbaroni.



Post a Comment