Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na madiwani na
watendaji wa Manispaa hiyo wakati wa kikao maalum cha kuahirisha Baraza
hilo kilichofanyika jana Dar es Salaam. Wengine ni Naibu Meya, Songoro
Mnyonge na Mkurugenzi wa Manipss hiyo, Eng. Mussa Nati (kulia).
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akimtambulisha Rais Mstaafu wa
awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi kwa Madiwani wa Manispaa hiyo
baada ya kuwasili kwenye ofisi za Manispaa hiyo kuhudhuria hafla maalum
ya kuahirisha Baraza hilo Dar es Salaam jana.
Ofisa
Kilimo (Umwagiliaji na Ushirika) wa Manispaa ya Kinondoni, Salehe Hija
Mohamed akimelezea Rais Mstaafu alhaj Ali Hassan Mwinyi kuhusu mazao ya
kilimo alipotembelea maonesho ya miradi mbalimbali ya Manispaa hiyo.
Rais
Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akimvisha nishani Diwani wa Hananasif,
Abbas Tarimba wkati wa hafla ya kuliahirisha Baraza la madiwani hao, Dar
es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda,
Naibu Meya, Songoro Mnyonge (kushoto), Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Raymind Mushi na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Eng. Mussa
Nati.
Rais
Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti chake mmoja wa
watumishi wa Manispaa hiyo, Deborah wakati wa hafla ya kuliahirisha
Baraza la Madiwani hao jana. Wanaoshuhudia ni Meya wa Manispaa hiyo,
Yusuph Mwenda, Naibu Meya, Songoro Mnyonge (kushoto), Mwakilishi wa Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymind Mushi na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,
Eng. Mussa Nati.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akionesha cheti cha Freeman
alichokabidhiwa na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto kwake)
katika hafla hiyo. Cheti hicho kinachotolewa na Baraza la Madiwani
hutolewa mara chache kwa Meya aliyefanikiwa kutekeleza miradi ya
wananchi kwa kiwango kikubwa na kina maana ya ‘Raia Huru’. Kushoto ni
Naibu Meya, Songoro Mnyonge na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Raymond Mushi.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akimkabidhi jezi ya timu ya Soka
ya Kinondoni (KMC FC) Rais Mstaafu alhaj Ali Hassan Mwinyi baada ya
kukabidhiwa kuwa Mlezi wa klabu hiyo kwenye hafla hiyo.
RAIS
Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni kwa mafanikio iliyoyapata katika kusimamia na kutekeleza
miradi yake kwa kiwango kikubwa.
Rais
Mwinyi alisema kuwa Manispaa hiyo ni ya mfano kutokana na kusimamia vema
miradi yake na kuitekeleza kwa kiwango kikubwa jambo ambalo ni tofauti
na Manispaa nyingine nchini.
Alisema
kuwa ongezeko la makusanyo kwa asilimia 360 kutoka shilingi Bilioni 10
hadi kufikia Bilioni 36 kwa mwaka na kuifanya kuwa Halmashauri ya kwanza
kuweza kusimamia miradi yake kwa fedha zake zenyewe pasipo kutgmea
ruzuku ya Serikali.
Rais
Mwinyi aliyasema hayo wakati wa hafla ya kuliahirisha Baraza la Madiwani
wa Manispaa ya Kinondoni iliyofanyika kwenye ofisi za Manispaa hiyo,
Dar es Salaam jana.
Aidha
aliipongeza Manispaa hiyo kwa kuweza kuwahamasisha wananchi wake wapende
usafi na hivyo kubadilisha kwa kiasi kikubwa mazingira ya usafi kwa
maeneo mbalimbali ya Manispaa hiyo.
“Nawashukuruni
sana ndugu zangu, mmenifanyia mengi sana mtaani kwangu, nyumba yangu
ilizungukwa na msitu, takataka, vumbi na kadhalika lakini leo nipo
katikati ya Barabara safi za lami, Napata hewa safi mimi na bibi yenu.”
Alisema kwa utani huku akicheka.
Kwa
upande wake Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda aliwaahidi wananchi wa
Manispaa yake kuendelea kushirikiana nao katika kuyaendeleza yale yote
waliyoyafanya kwa kushirikiana na Madiwani na Watendaji wa Manispaa hiyo
hata pale itakapotokea hawatarudi tena kwenye nafasi zao mwakani.
Aidha
alisema kuwa anajivunia mafanikio makubwa yaliyoipata Manispaa hiyo
katika kipindi cha uongozi wake ikiwemo kuongoza kati ya Halmashauri
zote nchini na pia kung’ara katika Majiji ya Kati.
Hata
hivyo Meya huyo aliwataka wananchi kuendeleza kampeni ya uwekaji safi
mazingira ya Manispaa hiyo ili kupuka maradhi mbalimbali
yanayosababishwa na uchafu.
“Haiwezekani
Kinondoni kuwa safi kama wewe mwananchi haupo msafi. Ni wajibu wa kila
mmoja kuhakikisha anasimamia vema maendeleo tuliyoyapata kwa faida yetu
na vizazi vyetu.” Alisema Meya Mwenda.
Hafla
ya kuliahirisha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ilikwenda
sambamba na utoaji wa vyeti na tuzo kwa Madiwani, watendaji na maafisa
wa idara mbalimbali za Halmashauri hiyo na kuhudhuriwa na viongozi wa
ngazi za juu Serikalini, Wawakilishi wa madhehbu mbalimbali ya kidini,
Wanasiasa na wananchi.
Katika
hatua nyingine, Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni limemtunuku Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda cheti cha
heshima cha Raia Huru ‘Freeman’ kwa kutambua mchango wake mkubwa katika
kuiletea maendeleo Manispaa hiyo.
Meya
huyo amekuwa ni wa kwanza kutunukiwa cheti hicho tangu kuanzishwa kwa
Halmashauri hiyo ambacho kinamfanya sasa kuwa raia huru na kumtambua
kama mtu aliyeleta mafanikio makubwa katika Manispaa hiyo na wananchi
wake kwa ujumla.


Post a Comment