

WENYE MSIMAMO
Wanawake
daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo,
uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao
na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.
WAPENDA USAWA
Aina
ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake
wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia
kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa
asilimia 50 kwa 50.
WANAOJUA MAPENZI
Wanawake wajuzi wa mambo
ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni uwezo wa kutosheleza
katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume hupenda sana
wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita. Mara nyingi wanatajwa
kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au
za ndani.
MARAFIKI
Wanawake
wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao
hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na
kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha
kwa wapenzi wao. Si wakorofi, waungwana na wapenda amani.
WA WAZI
Aina
nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na uwazi. Si
wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni
wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa
kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo.
WANAOJITEGEMEA
Wanawake
wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina naomba
vocha kila siku. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wa leo hawapendi
wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande
mmoja.
WASIO NA PRESHA
Nikisema wanawake wasiokuwa na presha
namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Wao siku zote
huacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya
majukumu yao kama wapenzi.
MARIDADI
Kundi lingine la wanawake
wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na kujiremba. Wanaokwenda
na wakati katika mavazi na mvuto wa nje. Lakini pia ni welewa wa
mazingira, si wasamba. Wanapendeza kwa muonekano.
WANAORIDHIKA
Wanawake
ambao hulidhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume, hili
ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa
wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda
chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema
ya mwanamke.
WA MMOJA
Wanawake wanaochagua mara moja na
kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa
wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua
mwanzo wanahitajika sana. “Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu
sitaki mtu mwingine.” Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu
sana.

on Wednesday, July 8, 2015
Post a Comment