Mwenyekiti
wa CCM, D.r Kikwete makamu mwenyekiti Philip Mangula (katikati) na
waziri mkuu Mizengo Punda wakifuatilia jambo. Tuhuma ambazo wamekuwa
wakimhusisha nazo ni pamoja na ufisadi, matumizi ya fedha katika
kutafuta uungwaji mkono na uanzaji kampeni mapema, mambo ambayo
yamewekewa zuio na CCM na hivyo kuwafanya wanaomjengea hoja za
kukataliwa kushikilia silaha hiyo kwa lengo la kumdhoofisha matumaini ya
kupitishwa na vikao vya chama
WAKATI
jina la waziri mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa likitajwa kila
kona katika kinyang’anyiro cha kusaka nafasi ya kuwania urais kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM), saa 48 zimesalia kufahamu kuwa jina la
mgombea huyo litakatwa au halitakatwa katika mchujo wa kwanza, Uwazi
linashuka nayo.
Waziri
mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa. Duru za kisiasa nchini
zinauangazia mkutano unaowahusisha wajumbe 32 wa Kamati Kuu (CC) ya
chama hicho utakaofanyika keshokutwa (Alhamisi) kuwa ndiyo utakaotegua
kitendawili cha wagombea gani watapenya kwenye hatua ya Tano Bora na
majina yao kupelekwa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) kwa ajili ya
kupigiwa kura ya awamu ya pili.
ITAKAVYOKUWA
Muongozo
wa kumpata mwakilishi wa nafasi ya urais kupitia CCM unaonesha kuwa,
majina ya wagombea watano yatakayopitishwa na CC yatachekechwa tena na
Nec na kuwapata wagombea watatu ambao watakwenda kupigiwa kura na
wajumbe wa Mkutano Mkuu ambapo mshindi mmoja atapatikana na
kukiwakilisha chama kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba,
mwaka huu.
ANAKATWA, HAKATWI YA LOWASSA INATOKA WAPI?
Pamoja
na kuwa ndiye mgombea anayeonekana ana nguvu kwa kuungwa mkono ndani na
nje ya chama chake, Lowassa amekuwa katika msukosuko mkubwa wa kisiasa
kutoka kwa mahasimu wake ambao wamekuwa wakifanya kila linalowezekana
kuhakikisha kwamba mwanasiasa huyo hapewi nafasi ya urais.
Hata
hivyo, wanaomuunga mkono pamoja na Lowassa mwenyewe wamekuwa akipuuza
madai hayo huku wakiwataka wanaoshabikia mambo hayo kuweka ushahidi wa
kutosha juu ya madai yao, la sivyo waache kufanya siasa za maji taka.
“Nimekuwa
mwana CCM tangu mwaka 1977 nilipomaliza chuo kikuu, sijawahi kufanya
kazi nje ya CCM. Hivyo nakijua chama na hakuna mgombea atakayeweza
kuvunja rekodi ya utendaji wangu katika chama. Sasa leo anayetaka kukata
jina langu anatoka wapi? Anakata kwa sababu gani?
Kinana.
“Sioni kosa la kukatwa jina na Watanzania hawaoni. Kwa hiyo msiwe na
wasiwasi jina litarudi tu,” Lowassa aliwaambia maelfu ya watu
waliojitokeza kumdhamini alipowasili mkoani Ruvuma hivi karibuni.
AKIKATWA ITAKUWAJE?
Mmoja
kati ya wafuasi wa Lowassa, ambaye amekuwa akijipambanua pia kuwa ni
msemaji wake, Hussein Bashe amewahi kunukuliwa akisema: “Kama CCM
watamkata Lowassa kwa hila watarajie kukutana na nguvu za umma.”
Ingawa
Bashe hakufafanua zaidi nguvu ya umma itafanya nini na kwamba mgombea
wao atafanyaje jina lake likiondolewa lakini duru za kisiasa zinaonesha
kuwa huenda chama hicho kikapata mtikisiko mkubwa kutokana na kile
kinachotajwa kuwa ni Lowassa kuwa na mtaji mkubwa wa watu wanaomuunga
mkono.
Katika
safari yake ya kusaka wadhamini, mgombea huyo amekuwa akitikisa kwa
kupata mapokezi makubwa karibu katika kila mkoa aliyokwenda ambapo
ameweza kujikusanyia zaidi ya wadhamini laki nane, ingawa wanaohitajika
na chama ni 450 tu kutoka katika mikoa 15.
Dr. Shein CHAMA KIKOJE?
Kama
ilivyo kwa jina lake kuondolewa, Lowassa bado anakiweka njia panda chama
chake kutokana na kuwepo kwa makundi ndani ya chama hicho ambayo
yanaonesha kuwa hayako tayari kumuunga mkono katika safari yake ya
kuingia ikulu.
Yeye
waziri mkuu wa zamani, Fredrick Sumaye ameshatangaza mgogoro na chama
chake endapo jina lake litaondolewa na kwamba yuko tayari kukihama chama
hicho kama dalili za kuwapendelea anaowaita mafisadi zinavyoonekana.
Mtazamo
huu, huenda ukaathiri umoja wa CCM tofauti na miaka ya nyuma endapo
chama kitaamua kumpitisha mgombea ambaye wenzake wanamchukulia kama mtu
asiyefaa kupewa nafasi hiyo, mwenyekiti wa chama na amiri jeshi mkuu wa
majeshi ya ulinzi na usalama.
SAA 48 ZIKO KWA HAWA
Pamoja
na mitazamo yote, wajumbe wa kamati kuu ambao macho na masikio ya wengi
yanawatazama na kusikia uamuzi wao kesho kutwa ni hawa wafuatao:
Wengine
ni Mohammed Seif Khatib, Zakhia Hamdan Meghji, Asharose Migiro, Sofia
Simba, Sadifa Juma Khamis, Abdallah Majura Bulembo, Jenista Mhagama,
William Lukuvi, Pindi Chana, Jerry Silaa, Adam Kimbisa, Shamsi Vuai
Nahodha na Hussein Mwinyi.
Mbali
na wajumbe hao, wapo pia Maua Daftari, Samia Suluhu, Salim Ahmed Salim,
Makame Mbarawa na Hadija Abood. Hata hivyo, katika kikao cha kuchuja
majina hayo, wagombea waliotangaza nia hawataruhusiwa kuingia kwenye
uteuzi wa majina.


Post a Comment