Akizungumza na wanahabari jana katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) Given Edward amesema yeye ni miongoni wa watanzania 9 waliokuwa wamechaguliwa na nchi za jumuiya ya madola ambazo zilitangaza kutengeneza ‘project’ mitandao ya kijamii ambapo aliibuka kidedea.
Alisema kuwa katika vijana hao 9 wa kitanzania aliweza kuibuka kuwa mshindi wa kwanza wa tuzo hizo zijulikanazo kama ’The Queenns Young Leaders’ ambapo alitengeneza project ya mtanadao ujulikanao kama ‘My Elimu’ ambao lengo lake ni kuwakutanisha wanafunzi pamoja kutoka nchi mbalimbali kuweza kusoma kwa kutumia mtandao huo pasipo kuwa sehemu moja.
“Mtandao huo ni nafuu sana kwa kizazi cha sasa kwani unamrahisishia mwanafunzi kuweza kujadiliana masuala mbaliambali ya kielimu, namana ya kukokotoa maswali bila kusafiri kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine pasipo bila kupoteza mda hivyo nawaombeni watu waufatilie”alisema.
Aliongeza kuwa kadiri siku zinavyokwenda anatarajia kubalidilisha mfumo wa maandishi kuwa katika picha ili kumwezesha mwanafunzi kuwa katika mfumo wa kileo wa teknolojia na hata kumwezesha aliyepo kijijini kuweza kupata maswali mbalimbali ya masomo papo hapo kwa kutumia mfumo huo wa My Elimu ambao ni wa haraka sana, hivyo akawataka vijana kutembelea mtandao huo wa www.MyElimu kuweza kujifunza zaidi.
HABARI, PICHA: NA DENIS MTIMA/GPL
Post a Comment