Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mwandishi wa habari, Mariam Mkubaru amefariki dunia.

Mwandishi wa habari, Mariam Mkubaru enzi za Uhai wake
--
Mkubaru alifikwa na umauti katika ajali ya gari inayodaiwa kutokea jana Ruangwa, mkoani Lindi akiwa katika shughuli zake.

Simu yake ilipojaribu kupigwa ili kupata ukweli wa tukio hilo, ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mama yake ambaye hata hivyo alishindwa kuzungumza kutokana na kulia.

Mkumbaru, amewahi fanyia kazi katika vyombo vya habari vya The Guardian Ltd, New Habari, Uhuru, Mzalendo, BBC, na baadae kuandikia mitandao ya kijamii Blogs.

Hadi anafikwa na umauti, alikuwa ni Mshauri wa Mradi wa Mama Yee unaotekelezwa na UTPC kupitia gazeti la Tuwasiliane.

Kifo hicho ni pigo lingine kwa tasnia ya Habari nchini Tanzania kufuatia mfululizo wa vifo vya waandishi vilivyotokea kwa mwaka huu ambapo vinadaiwa kufikia waandishi 7. 

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top