Kufuatia skendo ya utapeli inayoendelea kumwandama mwimbaji wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando anadaiwa kupigwa pingu mkoani Dodoma, baadaye akasafirishwa hadi Dar kwa msimamizi wa kazi zake, Alex Msama, kwa lengo la kumlipia deni alilokuwa akidaiwa.
Habari
kutoka kwa chanzo zimeeleza kwamba, hivi karibuni, Rose alilipwa Sh.
milioni 3 kwa ajili ya shoo huko Makambako mkoani Njombe na matangazo
yakafanyika lakini hakutokea.
Ikadaiwa
kuwa, wakati matangazo ya shoo yakiendelea, mtu mwingine aliyekuwa
akimdai Sh. milioni 3.5 (pia alichukua fedha kwa shoo siku za nyuma)
alikwenda Makambako kwa lengo la kumsubiri Rose ili amnase, lakini
hakutokea.
Chanzo
hicho kiliendelea kumwaga ‘unyunyuzi’ kuwa, wawili hao waliripoti ishu
ya Rose, Kituo cha Polisi Makambako ambapo polisi walifunga safari
kumfuata Dodoma.
Sosi
huyo alisema kuwa, Rose alikamatwa Juni 27, mwaka huu na kuswekwa
rumande Kituo Kikuu cha Polisi, Dodoma tayari kwa kupelekwa mahakamani.
Imedaiwa kuwa, kigogo mmoja wa serikali mkoani humo (jina lipo) aliwaambia polisi wampigie simu Msama na kumweleza kisanga hicho ili ikibidi yeye amlipie deni hilo kwa sababu anamsimamia kazi zake.
Imedaiwa kuwa, kigogo mmoja wa serikali mkoani humo (jina lipo) aliwaambia polisi wampigie simu Msama na kumweleza kisanga hicho ili ikibidi yeye amlipie deni hilo kwa sababu anamsimamia kazi zake.
“Msama
alikubali kwa sharti kwamba, kwa sababu ana kazi ya kufanya na Rose
hivyo asafirishwe hadi Dar amlimpie, yeye na Rose watakatana kwenye
kazi.
“Rose
alisafirishwa Juni 29, mwaka huu akiwa chini ya ulinzi wa askari
wawili. Mmoja wa kike ambaye alilala naye chumba kimoja hotelini. Kesho
yake wakaenda ofisini kwa Msama, Block 41, Kinondoni, akalipa milioni
sita na laki tano keshi,” kilisema chanzo.



Post a Comment