
SAKATA
la walimu wa Shule ya Msingi Nambaza iliyopo Jimbo la Mwibara, Wilaya
ya Bunda, mkoani Mara, kufanyiwa vitendo vya kishirikina wakidai
kuingiliwa kimwili, kuibiwa mali na fedha, sasa limechukua sura mpya.
Hali
hiyo inatokana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Joshua Mirumbe kuagiza
watuhumiwa (wachawi), ambao wananchi waliwabaini kuhusika na vitendo
hivyo kwa kupigiwa kura, wakamatwe haraka na kufikishwa katika vyombo
vya dola.
Mirumbe
alitoa agizo hilo jana ofisini kwake katika kikao ambacho
kilimshirikisha Mbunge wa jimbo hilo, Kangi Lugola, viongozi wa Serikali
ya Kijiji cha Nambaza na Kata ya Nansimo.
Alisema
vitendo vya kishirikina wanavyofanyiwa walimu hao ni udhalilishaji
mkubwa ambao hauwezi kuvumiliwa na kumlalamikia Ofisa Tarafa ya Nansimo,
Bw. Jonas Nyeoja kwa kuzembea na kutochukua hatua za haraka.
Alisema
Bw. Nyeoja alipaswa kuwakamata watuhumiwa 15 ambao wanalalamikiwa
kuwatesa walimu kwa kuwafanyia vitendo vya kishirikina na kuwafikisha
katika vyombo vya dola.
"Nimemuagiza
Ofisa Tarafa (Nyeoja), akawakamate watuhumiwa ambao orodha ya majina
yao ninayo na wafikishwe kwenye vyombo vya dola wakati tukiandaa maeneo
ya kuwahamisha kwani wamekosa sifa za kuishi kijijini hapo na wenzao
hawawataki," alisema.
Aliongeza
kuwa, kuendelea kuwakumbatia watu hao ni kusababisha machafuko kijijini
kwani upo uwezekano wa wananchi kuchukua sheria mkononi na kuwaweka
walimu katika hofu, kukosa molari wa kazi.
Kwa
upande wake, Bw. Lugola ambaye alilazimika kusitisha vikao vya bunge na
kwenda jimboni kwake kushughulikia tatizo hilo, akiwa katika mkutano wa
hadhara alioufanya kijijini hapo, alitokwa na machozi baada ya kuelezwa
jinsi walimu hao walivyofanyiwa vitendo vya kinyama kwa kuwadhalilisha
na kuwaondolea utu wao.
Katika
mkutano huo, wananchi mbali na kuwataja wahusika wa vitendo hivyo
hadharani, walimtaka Bw. Lugola ahakikishe watu hao wanahama haraka
jimboni humo kabla hawajachukua sheria mkononi hatua ambayo itakuwa na
madhara, umwagaji damu.
Bw.
Lugola aliwaeleza wananchi hao kuwa yuko pamoja nao ili kuhakikisha
watu hao wanahama jimboni kwake, lakini kwa kuwa hana mamlaka ya kufanya
hivyo kesheria, atalifikisha suala hilo kwa Mkuu wa Wilaya mwenye uwezo
wa kufanya hivyo kisheria.
Katika
mkutano huo, pia alikuwepo Diwani wa Kata ya Nansimo, Sabato Mafwimbo,
Ofisa Tarafa (Nyeoja), Ofisa Mtendaji Kata ya Nansimo, Bryceson
Mashauri, Mratibu Elimu Kata, Pius Kijoriga na Mwenyekiti wa Kijiji cha
Nambaza, Leonard Mtelalilwa.
Jana
Bw. Lugola aliongozana na viongozi hao pamoja na polisi kwenda kijijini
Nambaza kuwakamata watuhumiwa hao kutokana na agizo la Mkuu wa Wilaya
na kusema kama polisi watasita kuwakamata watuhumiwa kwa lengo la
kuwalinda, yeye atamkamata hadi mtu wa mwisho.
Watu
hao wanadaiwa kuwaingilia kimwili na kuwafanyia walimu vitendo hivyo
usiku wakiwa wamelala pamoja na kuchukua nyaraka zao mbalimbali zikiwemo
vitambulisho na kadi za benki (ATM) kwa njia za kishirikina.
Pia
wachawi hao wamekuwa wakijisaidia haja kubwa na ndogo katika vitanda
vya walimu hao, kuweka vyakula, unga na mboga na wakati mwingine walimu
hujikuta wamelazwa chini wakiwa utupu na chakula hubadilishwa
kishirikina ambapo kama walikuwa wakila wali na nyama ya kuku, ghafla
unakuwa ugali na maharage.
Post a Comment