Klabu ya
Arsenal imeanza vibaya msimu mpya wa Ligi Kuu ya England baada ya
kuchapwa mabao 2-0 na West Ham United Uwanja wa Emirates jioni ya leo.
Cheikhou
Kouyate alianza kufunga akitumia makosa ya kipa Petr Cech kuipatia West
Ham bao la kwanza dakika ya 43, kabla ya Mauro Zarate kufunga la pili
dakika ya 57.
Adrian
aliokoa michomo kadhaa ya hatari katika mchezo ambao kocha Slaven Bilic
alimtumia kinda wa miaka 16, Reece Oxford akicheza mechi yake ya kwanza
ya Ligi Kuu England.
Kikosi
cha Arsenal; Cech, Debuchy/Sanchez dk67, Mertesacker, Koscielny,
Monreal, Coquelin/Walcott dk58, Cazorla, Ramsey, Ozil,
Oxlade-Chamberlain na Giroud.
West Ham:
Adrian, Tomkins, Reid, Ogbonna, Cresswell, Oxford/Nolan dk79, Noble,
Kouyate, .Payet, Zarate/Jarvis dk63, Sakho/Maiga dk89.
Post a Comment