Kama umekua ni mfatiliaji wa muziki wa Hiphop kwa Tanzania inawezekana hii taarifa ikakushtua kutoka kwa mmoja wa wanafamilia wanaowakilisha kundi la Weusi anaitwa Bonta,Jioni ya Aug 16 Bonta amenitumia ujumbe kuhusu msimamo wake juu ya muziki wa Hip Hop aufanyao.
‘HIP HOP SASA IMETOSHA
nipo kwenye huu muziki wa HPHP toka mwaka 1997 mpaka leo ni takribani miaka 15!!
nimefanya ngoma mingi sana eg MATUSI, MTI WENYE MATUNDA, NAUZA KURA, MAUWONGO, B3, MAARIFA, NYERERE, MAKTABA, WALAUMIWA, MTAANI WATU BUU, MACHO YANGU nk ’
‘Sasa nimeamuwa kubadilika rasmi na kuingia kwenye muziki wa BONGO FLEVA nikifata kwa karibu kabisa nyayo za jaffarai, ney wa mitego, cyrill, shetta etc
wengi wataona kama nimesaliti HIPHOP la hasha naomba wanisamehe!! na najua marapa wengi watafurahia kuskia nimeanza kuimba BONGO FLEVA wakiamini upinzani unapungua, waambie wasianze kujipongeza muda bado!! ningependa niimbe RnB kama ben pol, damian, jux au rama d sema ile ni ngumu sana na inahitaji ufundi, basi mi ntaimba hii hii ya kubahatisha melody matata maneno 2 tatu watu kati,
kwa kuanza nitaachia wimbo wangu mpya unaoitwa MAPENZI MATAMU!!
Naomba nisihukumiwe mpaka hii ngoma itoke’.
Post a Comment