Nape Nnauye
Kamati
Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeteua wagombea tisa wa nafasi ya
ubunge katika majimbo ya uchaguzi tisa kati ya 11 yaliyorudia uchaguzi
Agosti 13, mwaka huu na kubariki kutoswa mawaziri watatu jumla.
Mawaziri hao ni walioshindwa katika kura za maoni za marudio.
Waliotemwa
katika uteuzi wa Kamati Kuu ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus
Kamani (Busega); Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid
(Rufiji) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk.
Biligith Mahenge (Makete).
Kamati Kuu ilikutana jana katika ofisi ndogo za CCM Lumumba, Dar es Salaam jana chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape
Nnauye, waliopitishwa niJerry Silaa (Ukonga), Edward Mwalongo (Njombe
Kusini), Venance Mwamoto (Kilolo), Dk. Raphael Chegeni (Busega) na Edson
Ngonyani (Namtumbo).
Wengine
ni Mohamed Mchengerwa (Rufiji), Dk. Norman Sigara (Makete), Martin
Msuha (Mbinga Vijijini) na Joel Makanyanga Mwaka (Chilonwa). Nape
aliyataja majimbo yaliyokuwa hayajatolewa maamuzi kuwa ni Jimbo la
Singida na Kiteto mkoani Manyara.
Nape
alisema mbali na kikao hicho kuteua majina ya wagombea, pia kilijadili
ajenda za uchaguzi mkuu ujao ambao utafanyika Oktoba 25, mwaka huu.
“Kura
za maoni siyo kigezo pekee cha kumpitisha mgombea kuwania nafasi ya
ubunge, hivyo kuna taratibu na kanuni za vikao mbalimbali vya chama,
tathmini imefanywa na kusimamisha hawa, tumekuwa tukibadilisha taratibu
za kupata wagombea ubunge mara kwa mara,” alisema Nape.
Post a Comment